Michezo

Video: Mchezaji wa Everton ajifunza kupika Ugali

Mchezaji wa klabu ya Everton ya Uingereza, Phil Jagielka ameamua kujifunza kusonga Ugali hii ni mara baada ya kuwasili nchini na timu yake kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia utakao pigwa leo jioni.

Mchezaji wa klabu ya Everton, Phil Jagielka

Kikosi kizima cha Everton kimeonekana kujifunza mapishi mbalimbali kama vile mchicha, nyama ya mchuzi, bamia, nyanya chungu vikionekana kukarangizwa na wachezaji hawa maarufu.

Jagielka amejiunga na wenyeji hao wa Goodson Park mwaka 2007 akitokea Sheffield United kwa dau la pauni milioni 4 na kukabidhiwa unahodha mara baada ya kustafu kwa mchezaji Phil Neville.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents