Burudani

Video: Mr. Blue, Dayna, Barnaba Boy na Amini warekodi wimbo wa kampeni ya ‘Dereva Makini 2014’

Ni ukweli usiopingika kuwa ajali zimekuwa ni mwiba mchungu kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla unaoacha kilio, walemavu, yatima, wajane na wagane kila kukicha.

Katika kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali barabarani wakali katika muziki wa bongo fleva Mr Blue, Amini, Banaba Boy na Dyna Nyange wameshiriki kurekodi wimbo wao utakaotumika kwenye kampeni ya dereva makini inayolenga kuhamasisha uzingatiaji wa usalama barabarani na kwenye vyombo vya usafiri.

“Kwa kweli hili janga limekuwa kubwa sasa hivi, ukiangalia idadi ya watu wanaofairiki au kupata matatizo kila mwaka imezidi kuwa kubwa janga hili imezidi, nawashauri madereva kuwa makini wanapoendesha magari,” Mr Blue aliiambia blog ya Tabia nchi.Naye Amini alisema: Familia nyingi zinapotea kutokana na ajali zikiwa pamoja safarini, na ajali nyingi zinasababishwa na madereva, kutokuwa makini wanapokuwa wanaendesha magari yao.”

“Vizazi vingi tunavyotegemea ndio vije kuwa viongozi ndio wanapata ajali, ndo vianvyooangamia kwakuwa havina upeo wa kuepuka mambo kama hayo,” alisema Barnaba.

Wimbo huo umerekodiwa na mtayarishaji wa muziki C9 anayesema: Mimi mwenyewe binafsi nimeshapoteza ndugu yangu, nimepoteza nguvu kazi nyingi sana za wasanii ambao nilikuwa nategemea wangekuja kurekodi na kunipatia kipato.

Naye Dayna anasema,”Tunandugu zetu, wasanii wenzetu wanapata ajali na ajali nyingi zinatokana na uzembe kabisa, kwa hiyo nimejitoa kufikisha elimu ya dereva makini ili kupunguza ajali hizo.”

1620955_578388235570320_866503781_n

Kampeni hiyo ya dereva makini imeandaliwa na Transevents Marketing kwa lengo la kutoa hamasa kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kuwawezesha abiria kufika salama waendako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents