Burudani

Video: Ommy Dimpoz aeleza mabadiliko yaliotokea kwenye mwili wake baada ya upasuaji mkubwa ‘Nilikaa ICU wiki 3’

Msanii wa muziki, Ommy Dimpoz bado yupo nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa baada ya kupata matatizo katika mfumo wake wa kumeza chakula na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuubadilisha mfumo huo.

Akizungumza na Millardayo nchini Afrika Kusini, Ommy Dimpoz ameweza kusimulia namna upasuaji wake ulivyofanyika na kusababisha kukaa Chumba cha Uangalizi Maalumu ICU kwa muda wa wiki tatu baada ya mapafu yake kuleta shida.

“Baada ya kufanyiwa upasuaji kulikuwa kuna matatizo, mapafu yakawa hayafanyi kazi vizuri, kwahiyo baada ya kutoka kwenye upasuaji nikapelekwa ICU (chumba cha wangojwa mahututi) hali ilibadilika kwa sababu upasuaji walisema ni masaa 4 lakini yakaenda mpaka masaa 11. Kwa hiyo nikaa ICU kwa wiki tatu baada ya pale nikahamishiwa wodi ya wangonjwa ya kawaida muda ukafika wakaniruhusu bwana unaweza kwenda lakini unatakiwa kurudi baada miezi 3,”

Kuhusu sauti kubadilika alisema, “Side effect ya upasuaji huu sauti inaweza kwenda na kurudi, kwahiyo hivyo vitu tayari nilishaambiwa. Sometime nakuwa nipo fresh some time ndio inakuwa hivyo lakini wakati nipo mapumzikoni Kenya nilijaribu kuingia studio. Mabadiliko mengine tumbo langu sasa hivi limeamishwa limevutwa juu, kwahiyo hata nikila nashiba haraka nikila kidogo,”

Muimbaji huyo amesema bado hajajua ni sumu ya aina gani ambayo ametumia au amelishwa.

Katika hatua nyingine amesema baada ya kufika hospitali nchini Afrika Kusini safari hii aliwaeleza madaktari jinsi anavyojisikia na kufanyiwa vipimo.

“Walivyonipima wakakuta ndani kuna usahaa mwingi sana, akaseama inabidi tukutoboe pembeni ya tumbo tuunyonye, kwahiyo kuutoa siku ya kwanza wakatoa lita moja, wakaendelea mpaka mambo yakaa sawa,” alisema Ommy.

Related Articles

13 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents