Videos

[Video] Prezzo Aongea Exclusively Na Bongo5

Msanii Jackson Makini almaarufu kama Prezzo amefanya interview na Bongo5.com na kueleza kuwa kwa sasa anatoka kama brand mpya ya ki Afrika ambapo anajiandaa kufanya mambo yanayoendana na status ambayo ameipata baada ya kuingia jumba la Big Brother StarGame 2012.
Akizungumzia hali yake ya kimuziki Prezzo alisema muda si mrefu ataachia ngoma yake na pia siku si nyingi ataelekea makao makuu ya taasisi ya kijamii One Campaign Organization jijini New York nchini Marekani kwa ajili ya kupigwa msasa wa namna atakavyo fanya kazi zake za kijamii za kutokomeza njaa barani Afrika kama balozi rasmi wa One campaign.

Pia katika mahojiano hayo Prezzo alizungumzia kuhusu kupewa ofa za kushiriki muvi nchini Nigeria na kwamba amewaachia wanasheria wake wapiti e mikataba na proposal ambazo alipewa kabla ya kuchukua uamuzi stahiki. Akizungumzia sababu hasa iliyomfanya aende Nigeria Prezzo alisema alikwenda kule kama sehemu ya kwenda kuwaomba msamaha watu wa Nigeria kwa namna ambavyo anahisi uhusiano wake na Goldie uliwakera hasa hasa baada ya yeye kufarakana na Goldie na baadae kupelekea kutolewa katika shindano hilo.

Unataka kujua Prezzo aliongelea nini kuhusu Goldie na hatima ya uhusiano kati yake na aliyekuwa mshiriki mwenzake katika jumba la Big brother 2012.

Angalia interview hiyo hapa chini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents