Video: Producer Swizz Beatz wa Marekani azipa shavu ngoma mbili za Diamond

Producer mkongwe aliyewaingiza kwenye ramani ya muziki rappers maarufu wakiwemo EVE na DMX, Kasseem Dean maarufu kama Swizz Beatz wa nchini Marekani, ni shabiki wa nyimbo za Diamond Platnumz.

Producer huyo ambaye pia ni rapper na mume wa Alicia Keys, jana aliendelea kuonesha mapenzi yake kwa muziki wa Afrika kwa kupost video za mwanae pekee wa kike, Nicole Dean akicheza nyimbo za wasanii wa Afrika akiwemo Black Coffie na Diamond.

Nicole ni mtoto wa tatu wa Swizz aliyezaa na muimbaji wa Urusi Jahna Sebastian, anayeishi jijini London. Pia ana watoto wakubwa Prince Nasir Dean aliyezaa na Nicole Levy na Kaseem Jr aliyezaa na mke wa zamani Mashonda Tifrere. Pia ana watoto wawili na Alicia Keys, Egypt Daoud na Genesis Ali Dean.

w630_012315SwizzBeatzNicoleDean-1422050522
Swizz na mwanae Nicole

Kwenye video hiyo inayomwonesha Nicole akifurahia wimbo wa Diamond, Nana, Swizz aliandika: Vibes song by @diamondplatnumz #goodvibes.”

Hakuishia hapo, katika kuonesha kuwa anamfahamu vyema Diamond, Swizz alishare video nyingine akiwa na mwanae huyo wakisikiliza wimbo wa kitambo wa staa huyo ‘Nataka Kulewa’ na kuandika: Last one [joy] showing me her dance music by @diamondplatnumz it’s very important that our kids know the culture of music, Art & Life.”

Diamond amepokea kitendo hicho kwa furaha na heshima kubwa. Kupitia Instagram, ameshare video ya pili ya Swizz na kuandika: Thanks alot my brother @therealswizzz for keep Supporting Good Music…pass my greetings to your Beautiful Daughter #BongoflavourTotheWorld.”

Si mashabiki pekee wa Diamond na wapenzi wa muziki wa Tanzania waliofurahia shavu hilo, bali pia wasanii wenzake.

“This is Africa,, nafikiri bado tuna material nyingi za kutosha kwenye huu ulimwengu wa burudani AFRICA STAND UP WAMESHATUELEWA. Big up son @diamondplatnumz,” ameandika rapper wa Weusi, G-Nako.

Swizz Beatz ni miongoni mwa watayarishaji wa muziki wanaoheshimika sana nchini Marekani. Ametayarisha hits nyingi zikiwemo Party Up (Up in Here) ya DMX, Check on It na Ring the Alarm za BeyoncĂ©, Good Times ya Styles P, Bring ‘Em Out ya T.I, Hotel, I’m a Hustla za Cassidy, Touch It ya Busta Rhymes na zingine.

Kanye West aliwahi kumuita Dean kama ‘the best rap producer of all time.’

Related Articles

Back to top button