Habari

Video: Tume ya Maadili yapokea malalamiko ya Meya wa Ubungo, Jacob dhidi ya RC Makonda

Diwani wa kata ya Ubungo na ambaye pia ni mstahiki Meya wa Manispa ya Ubungo, Boniface Jacob amejibiwa barua yake ya malalamiko na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Machi 22 mwaka huu, Diwani huyo aliwasilisha mashitaka yake dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma na kukosa sifa yakuwa kiongozi.

Akiongea na waandishi wa habari Alhamisi hii, Boniface Jacob alisema amemshtaki RC Makonda kwa makosa tano huku moja wapo likiwa ni madai ya kufoji vyeti.

“Jana Aprili 12, nilipokea barua kutoka kwa Kamishna wa Tume, Jaji Harold R Nsekela akinijulisha kuwa Tume ya maadili ya viongozi wa Umma imekubali mashtaka yangu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, na kunitaarifu kuwa wameanza kuyafanyia kazi mashitaka yote,” alisema Jacob.

“Taarifa hiyo ya Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imetoa mwanga mkubwa kwamba haki ambayo wengi wamekuwa wakiiomba, sasa mwanga umeanza kuonekana. Hivyo niwaombe wapenda haki wote popote walipo tushirikiane kwa hili.Tupeane ushirikiano wa kuniongezea vielelezo vingine zaidi ya vile nilivyowasilisha tume yaani vyeti na nakala zingine za mali kama nimesahau jambo lolote.,” aliongeza.

Alisema muda wowote kuanzia sasa ataitwa na tume huyo kwa ajili ya kesi hiyo huku akiwataka wananchi wenye vielelezo dhidi ya tuhuma zinazomkabili kujitokeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents