Burudani

Video ya ‘Hallelujah’ ya Diamond Platnumz yaweka rekodi mpya barani Afrika

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amelishangaza bara la Afrika kwa kuweka rekodi mpya kupitia video ya wimbo wake mpya wa Hallelujah aliyowashirikisha kundi la Morgan Heritage kutoka Jamaica.

 

Video hiyo iliyowekwa jana usiku mpaka sasa hivi imetazamwa na watu milioni 1 ndani ya masaa 15.

Awali video ya muziki iliyokuwa inashikilia rekodi ya kutazamwa mara nyingi kwa muda mfupi barani Afrika ilikuwa ni ‘Closer’ ya Wizkid ambayo ilitazamwa na watazamaji milioni 1 kwa masaa 23.

SOMA ZAIDI-Video ya ‘Seduce Me’ ya Alikiba yavunja rekodi ya ‘Salome’ ya Diamond Platnumz

Kwa upande wa Tanzania hii inakuwa ni video ya kwanza kutazamwa na watu milioni 1 ndani ya siku moja. Je, kwa spidi hii video ya wimbo wa ‘Hallelujah‘ itavunja rekodi ya wimbo wa Davido ‘IF‘ kwa kufikisha views milioni 20 ndani ya mwezi mmoja?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents