Habari

Vodacom, CRDB kuongeza upatikanaji wa simujanja nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Abdulmajid Nsekela, wakipiga makofi mara baada ya kuzindua ushirikiano kati ya taasisi hizo unaoenda kuwezesha upatikanaji wa simujanja kwa mkopo ili kuchochea matumizi ya intaneti na ukuaji wa uchumi wa kidijiti nchini. Kulia kwa Besiimire ni Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Bi. Linda Riwa na kushoto kwa Nsekela ni Afisa Biashara Mkuu wa benki hiyo Bw. Boma Raballa.

Katika jitihada za kuongeza upatikanaji na matumizi ya simu janja ilikuziba pengo la kidijitali nchini, makampuni ya Vodacom Tanzania PLC na Benki ya CRDB wamezindua mpango wa kuwezesha Wateja wao kumiliki simujanja zenye ubora kwa gharama nafuu.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo wakukopesha simu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, alieleza kuwa kampuni hiyo ya simu inatekeleza mipango mbalimbali ya kupunguza gharama za vifaavya mawasiliano ili kuwawezesha wateja wake kuhamakutoka kwenye matumizi ya mtandao wa 2G na kumilikisimu zenye uwezo wa 4G na kutumia fursa hiyo ilikunufaika na faida kemkem zinazopatikana kupitiamtandao huo.

Tukiwa ni mdau na mshirika mkubwa wa sekta ya mawasiliano na teknolojia, Vodacom tunajivunia kuzindua mpango huu na Benki ya CRDB ambayo nitaasisi kubwa ya fedha nchini. Ushirikiano wetu unalenga kuwawezesha wateja kutoka pande zote mbilikupata aina mbalimbali za simujanja kwa bei nafuu na mpango wa malipo kwa awamu kwa kipindi fulani. Ili kujua kama amekidhi vigezo, mteja atatakiwa kupiga*150*00*44# nbaada ya hapo atafanya malipo ya awalina kupewa simujanja. Mkopo huu unaweza kulipwa kwasiku, kwa wiki au kwa mwezi kwa kipindi cha hadi miezi 12 kupitia M-Pesa,” alifafanua bwana Besiimire.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema, “ushirikiano huu baina yetu na Vodacom ni fursa nzuri kwa Watanzaniakupata huduma za kifedha na mawasiliano kwagharama nafuu. Kwa hiyo kama wadau muhimu tunapaswa kuunga mkono juhudi za Serikali ilikuhakikisha wananchi wake wanafaidika na ukuaji namaendeleo katika sekta hizi.

Bwana Nsekela aliongeza kuwa, “Kwa mtandao wetuulioenea nchi nzima, CRDB tumekuwa na mchango muhimu katika maendeleo ya Watanzania kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha. Hivyobasi, kwa kushirikiana na Vodacom, tutaweza kutoamchango wetu ili kuongeza matumizi ya simujanjanchini.”

Licha ya juhudi za mamlaka nchini kusogeza huduma za mawasiliano, wananchi wengi bado wanatumia hudumaza mtandao wa 2G. Hii inapunguza upatikanaji wa fursa zilizopo mtandaoni pamoja na kufurahia na kunufaika na intaneti yenye kasi zaidi kutoka Vodacom pamoja na bidhaa nyingine za kidijitali.

Matumizi ya simujanja na intaneti yana faida kwa jamii kama vile kukuza ukuaji wa kiuchumi kwa kuwezesha ujasiriamali wa kidijitali na kuchochea uvumbuzi, utafutaji masoko mitandaoni pamoja na kuongeza kipatokwa wananchi wanaoamua kujiajili kupitia dijitali.

Vodacom Tanzania imekuwa ikishirikiana na watengenezaji mbalimbali wa simu za mkononi na taasisi za kifedha ili kuwezesha Watanzania kumiliki simu kupitia mikopo nafuu na mipango rafiki ya malipo kwa mteja.

Mwezi August 2020, Vodacom ilizindua programu ambayo inawaruhusu wateja wake kumiliki simujanja kupitia mkopo unaolipwa kwa awamu, huku kianziokikiwa ni Shilingi 20,000 za Kitanzania kwa muda wa miezi 12.

Bwana Nsekela alimalizia kwamba anaamini kuwa taasisi hizo mbili zina huduma mbalimbali za kibunifuambazo zitawanufaisha na kuboresha maisha ya wateja wao. Pia alitoa wito kwa Watanzania wanaotumia simuza kawaida na wanataka zenye ubora zaidi kufika katikamaduka ya Vodacom na kupata simujanja kwa bei nafuuili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa kidijitali duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents