FahamuHabari

Nepi za watu wazima zina soko kubwa kuliko za watoto Japan

Kiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza nepi kwa ajili ya watoto wachanga nchini humo na badala yake kitaangazia soko la watu wazima. Oji Holdings ndiyo kampuni ya hivi punde kufanya mabadiliko kama haya nchini Japani yenye idadi kubwa ya wazee, ambapo viwango vya kuzaliana viko chini sana.

Mauzo ya nepi za watu wazima yalizidi yale ya watoto wachanga nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja. Idadi ya watoto waliozaliwa nchini Japani mwaka 2023 – 758,631 – ilipungua kwa 5.1% kutoka mwaka uliopita.

Pia ilikuwa idadi ndogo zaidi ya watoto waliozaliwa katika rekodi nchini Japani tangu Karne ya 19. Katika miaka ya 1970, idadi hiyo ilikuwa zaidi ya milioni mbili.

Katika taarifa, Oji Holdings ilisema kampuni yake tanzu, Oji Nepia, kwa sasa inatengeneza nepi milioni 400 za watoto wachanga kila mwaka. Uzalishaji umekuwa ukishuka tangu 2001, wakati kampuni ilipofikia kilele chake cha nepi milioni 700.

Huko nyuma mwaka wa 2011, mtengenezaji mkuu wa nepi nchini Japan, Unicharm, alisema mauzo yake ya nepi za watu wazima yamepita yale ya watoto wachanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents