Habari

Waliomuua Dereva wa Utalii Karatu wakamatwa

Jeshi la Polisi limesema kifo cha Dereva wa watalii, Omary Saimon, Msamo kilichotokea Wilayani Karatu, Machi 16, 2024 kimetokana na kuuawa ambapo Anthony Paskali (Lulu) na Emmanuel Godwin Joseph wakazi wa karatu wanashikiliwa kwa mauaji hayo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David, Misime amesema “Waliohusika walilenga kumpora, watuhumiwa wamekamatwa na wamekutwa na simu ya marehemu ila fedha walizompora Tsh 200,000 walikuwa wameshagawana na kuzitumia, walimpora baada ya kumpiga na kitu kisogoni na kudondoka chini.”

Awali ilidaiwa kifo hicho kimetokana na Askari Polisi kumjeruhi Omary baada ya kukamatwa njiani akituhumiwa kuendesha gari akiwa ametumia kilevi. Misime amesema Jeshi la Polisi linatoa tahadhari juu ya kueneza taarifa za uongo, chuki na uzushi dhidi ya mtu mwingine au Taasisi.

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents