Burudani

Wakili wa P Diddy aongea ukweli

Uongozi wa P Diddy umetoa taarifa juu ya msako uliofanywa Jumatatu, Machi 25 na mawakala wa Usalama wa Taifa kwenye nyumba mbili za msanii huyo ikiwemo ya Los Angeles na Miami, kuwa ulikuwa ni matumizi mabaya ya nguvu.

Msako huo ulifanywa baada ya msanii huyo kuhusishwa na madai ya biashara ya ngono yanayomkabili msanii huyo. Hivyo basi kwa mujibu wa tovuti ya Business Insider, imeeleza kuwa imepokea taarifa kutoka kwa wakili wa P Diddy aitwaye Aaron Dyer ikielezwa kuwa msanii huyo hakuwa na hatia hivyo msako uliofanywa kwenye makazi yake ulikuwa ni utumiaji mbaya wa nguvu za kijeshi huku akitaja vitendo hivyo kama chuki na uhasama.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa kilichofanyika ni uhasama kupita kiasi uliooneshwa na mamlaka hasa jinsi watoto na wafanyakazi wake walivyofanyiwa, hata hivyo taarifa hiyo imeeleza licha ya uvumi wa vyombo vya habari, si P Diddy wala mtu yeyote wa familia yake ambaye amekamatwa na uwezo wao wa kusafiri haujazuiliwa kwa njia yoyote ile.

Mbali na taarifa hiyo ya wakili vyombo mbalimbali nchini humo vimeripoti kuwa P Diddy ameuza hisa zake zote za kampuni yake ya Revolt TV kwa mtu asiyejulikana.

P Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono tangu mwaka jana 2023, kati ya waliowahi kumtuhumu ni aliyekuwa mpenzi wake Cassie.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents