Makala

Unafaa kufanya nini unapokutana na simba??

th

Mashambulizi ya wanyama wanaokula nyama dhidi ya binadamu ni nadra, lakini yamekuwa yakiongezeka tangu miaka ya 1950

Je unafahamu cha kufanya ikiwa utakutana na simba wa mlima(Mountain Lion) – na jinsi utaratibu unavyotofautiana na ule wa wanyamapori wengine?

Shambulizi la simba wa mlimani hivi majuzi huko California nchini Marekani limesababisha mwindaji mmoja kuuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya.

Kulingana na taarifa ya Ofisi ya Sherif wa Kaunti ya El Dorado , kijana mmoja alipiga simu kwa mamlaka mapema Jumamosi asubuhi na kuripoti kwamba yeye na kaka yake mwenye umri wa miaka 21 walishambuliwa walipokuwa wakifanya uwindaji.

Mamlaka ilifika eneo la tukio na kumpata kijana aliyejeruhiwa mwenye umri wa miaka 18 kabla ya kumpata kaka yake aliyekuwa chini karibu na simba huyo wa mlimani.

Ofisi ya Sherrif inaripoti kuwamaafisa wao walifyatua risasi hewani ili kuwatisha simba wa milimani na kukimbilia ndani kutoa msaada wa matibabu. Hata hivyo, walimkuta kijana huyo amefariki dunia kutokana na majeraha yake.

Mashambulizi ya simba wa mlima (pia huitwa pumas, panthers au cougars, kulingana na eneo ulilopo) ni nadra.

Bado, hili ni tukio la pili la kuogofya linalohusisha mnyama huyo kugonga vichwa vya habari nchini Marekani katika wiki za hivi karibuni.

Mnamo tarehe 17 Februari, marafiki watano walipigana na aina nyingine ya simba wa mlimani -cougar katika Jimbo la Washington: Marafiki walikuwa wakiendesha baiskeli kwenye mfumo wa njia wa Tokul Creek karibu na Fall City, kaskazini-magharibi mwa Snoqualmie chini ya Milima ya Cascade wakati mnyama huyo alipomshambulia mwanamke mwenye umri wa miaka 60 huko.

Wakifanya kazi pamoja, waendesha baiskeli waliweza kumbana simba wa mlima chini kwa baiskeli hadi msaada ulipowasili. Kwa bahati nzuri, mwanamke huyo alinusurika.

Shambulio mbaya la simba katika eneo hilo halijafanyika tangu 2018 . Na mara ya mwisho simba wa milimani kumuua mtu huko California ilikuwa miongo miwili iliyopita, wakati mwanamume mwenye umri wa miaka 35 aliposhambuliwa katika Hifadhi ya Mkoa ya Whiting Ranch katika Kaunti ya Orange.

Tangu mwaka wa 1890, kumekuwa na chini ya mashambulizi 50 ya simba wa milimani dhidi ya binadamu huko California – sita kati yao yakiwa ya kuua.

Kuongezeka polepole katika mashambulizi ya simba wa mlima

Hata hivyo, kumekuwa na ongezeko la mara kwa mara katika mashambulizi ya wanyama kwa wanadamu katika miaka ya hivi karibuni. Utafiti uliochapishwa mwaka wa 2023 katika jarida la PLOS Biology uligundua kuwa mashambulizi ya wanyama wanaokula nyama yameongezeka tangu miaka ya 1950, huku Afrika na Asia zikiwa na visa vilivyoongezeka zaidi.

Sehemu ya sababu hiyo ni kupunguzwa kwa makazi asilia kutokana na ongezeko la joto duniani . Wakati huo huo, wanadamu wanazidi kuingia katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa yanamilikiwa na wanyamapori kadiri idadi ya watu inavyoongezeka.

th
Ikiwa simba wa mlima atashambulia, njia ya kujiokoa ni kupigana kwa bidii uwezavyo

Mwalimu wa biolojia na wanyamapori Isabel McClelland ametunza wanyama wa Pori barani Afrika,kuhudumu kama mlinzi katika Hifadhi ya wanyama ya Maryland, ameratibu programu za elimu ya sayansi katika shule nchini Ghana, na alisoma kuhusu tabia za wanyamapori katika msitu wa Amazon wa Peru.

Anasema kwamba wanyama wanaokula nyama hawataki kutangamana kabisa na wanadamu na kwa kweli hufanya juhudi za kukaa mbali nao. “Ndiyo maana mashambulizi hayafanyiki mara kwa mara,” anasema.

Kwa kuzingatia hilo, wanyama wanaokula nyama, wakiwemo simba wa milimani, ambao kihistoria wameona watu wachache wanaweza kuogopa wanapokutana nao. “Walikuwa hapo kwanza, na wanalinda eneo lao,” McClelland anaelezea.

McClelland anasema kuwa pamoja na masuala kama vile kuongezeka kwa idadi ya watu, pia kumekuwa na ongezeko la idadi ya wasafiri – ikiwa ni pamoja na waendesha baiskeli, watalii na wawindaji – wanaotalii mbuga za kitaifa na maeneo mengine ya asili . Kwa hivyo, anasema juhudi za kufanya kuishi pamoja zaidi kwa njia “heshima na usawa” zinakuwa muhimu zaidi. Na kwa “juhudi”, anamaanisha sana elimu na uhamasisho .

Wanadamu wanapaswa kufanya nini ikiwa watakutana na simba wa mlima?

Hakuna mbinu moja ambayo ni tosha ya kushughulika na wanyama pori. Lakini Dk. Rae Wynn-Grant, Mtaalamu wa Ikolojia ya Wanyamapori na mwenyeji Mwenza wa Mutual of Omaha’s Wild Kingdom Protecting the Wild, anasema unaweza kuja ukiwa tayari. “Ninapendekeza kujijulisha na tabia na makazi ya simba wa milimani ikiwa unaishi au unapanga kutembelea maeneo ambayo wapo na kuwa makini sana,” anasema. Pia anashauri kubeba vijiti au vitoa kelele “ili usimshtue mnyama na kuwapa muda wa kutosha wa kuondoka kutoka kwako”.

Keith Bensen, mwanabiolojia wa wanyamapori katika Huduma ya Hifadhi ya Kitaifa, asema kwamba kuepuka kupanda milima peke yako ni shauri zuri la kufuata ukiwa nje, pia.

Bado, taratibu zingine hutofautiana kutoka kwa aina moja ya mnyama hadi mwingine. Kwa kawaida, simba wa mlimani atakimbia mara moja anaposikia au kuona binadamu, Bensen anasema. Ikiwa hatokimbia chaguo lako bora ni kuwa kuonekana kama tishio iwezekanavyo.

“Tunapendekeza kumkabili simba, kujifanya kuwa mrefu, kupiga kelele, kupunga mikono na kwa ujumla kujifanya uonekane wazi,” anaeleza. “Kisha rudi nyuma huku ukitazamana na mnyama, polepole, ukitoa kelele na kupunga mikono au mavazi yako wakati wote.” Anasema mnyama kukushambulia itakuwa “nadra sana” lakini ikiwa hilo litafanyika basi “kupigana kwa bidii iwezekanavyo” kwani ndilo chaguo lako bora.

Pendekezo hilo ni muhimu kukumbuka, haswa kwa sababu ni ushauri sawa kabisa unapaswa kufuata unapokutana na dubu mweusi(Black bear), Bensen anasema. Lakini, hasa, si sawa kwa kila aina ya dubu.

Ingawa aina fulani za dubu wa kahawia (grizzly) zimetoweka , Grizzly wa Amerika Kaskazini bado anaweza kupatikana – katika maeneo mengi ya Amerika Kaskazini (hasa huko Alaska, Montana, Idaho, Wyoming, Washington na Kanada). Dubu wa kahawia (Brown Bear) hawaogopi kirahisi kama dubu weusi, kwa hivyo usijaribu kuwatisha, na hupaswi kukimbia, kulingana na Kamati ya Interagency Grizzly Bear , shirika la Montana linalojitolea kurejesha na kuhifadhi dubu hao. Badala yake, jitahidi utulie na urudi nyuma polepole. Dubu akikushambulia, usipigane naye – jifanye tu kama uliyekufa.

Mashambulizi ya wanyama hutokea, lakini wataalam wana wasiwasi kuhusu kuenea kwa habari zisizo sahihi. McClelland anasema kwamba tunapoona mashambulizi ya wanyama katika habari, inaweza kuwa rahisi kudhani kwamba wanyama wanaokula nyama, ikiwa ni pamoja na simba wa milimani, ni viumbe wabaya, wenye ukatili kwa asili na wakali wakati sivyo. Kwa kweli, wanataka tu maeneo yao yaheshimiwe, na inawapasa wanadamu kuzingatia hilo.

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents