Bongo5 ExclusivesBongo5 MakalaBurudaniFahamuLifestyleMakalaMapenziUmbea

Mh. Hamisi Kigwangalla aamua kuwaambia ukweli vijana

For boys (na Labda wasichana pia wanahitaji kusikia haya! ):

1. Hakikisha unaoa. Kuoa ni lazima. Kuoa siyo lazima uwe na pesa. Ukikua kiasi cha kuzalisha mwanamke, oa! Mengine yatajipanga. Uoe nani sasa, sikia mtazamo wangu!

2. Oa tu mwanamke kama unampenda na una nia ya kuanzisha familia iliyo bora. Oa mwanamke atakayekuwa rafiki mzuri kwako na mama mwema kwa wanao. Oa mwanamke mwenye MUNGU ndani yake. Ni bonus ukipata mwenye shape, lakini lazima awe na Mungu ndani yake.

3. Ikitokea ukaoa usiwe mwepesi kutoa talaka. Ipambanie ndoa yako isimame. Hakuna viumbe wagumu kuwaelewa kama wanawake. Wanadamu tuko wawili tu – Ke na Me! . Lakini Ke my brother, ni mgumu sana kumuelewa. Ukiishaamua kumuoa, jifunze kumvumilia, kumhurumia, kumpuuza (akianza maneno, maana kwa uhakika ataanza tu!)

4. Usije ukarogwa hata siku moja ukamuoa msichana ambaye ana MENTALITY, ya kuwa eti Wewe ni chanzo chake cha pesa na maisha mazuri; ila zingatia tu kwamba wanawake wote duniani watakupenda na kukukubali kama una pesa!

5. Jua kwamba ni jukumu lako kumhudumia mwanamke wako, lakini mwanamke aliye bora ni yule asiye na mentality ya kukuchuna, ni yule mpiganaji anayezalisha chake, anayeweza kukizalisha chako/chenu na anayeweza kukusaidia kujenga maisha ya familia yenu.

6. Mwanaume kamili aliye bora haulizi kipato cha mkewe, hamgawii mwanamke majukumu ya familia (hata kama mwanamke ana kipato kikubwa kuliko yeye). Zingatia neno ‘mentality’ ya kiume. Na mentality ya ‘kike’! Kaa kwenye mentality yako, ila kama ulichagua mwanamke sahihi, ata-step in kuinyanyua familia na hali ya maisha yenu bila kuambiwa, bila kulalamika, kwa siri na staha kubwa, na bila kukudhalilisha.

7. Epuka kukaa kwenye mahusiano na mwanamke anayekuomba nauli kila siku mkitaka kwenda out, anayekuomba pesa ya salon kila mkitaka kutoka, anayelewa pombe sana, anayependa kuwasiliana na kujenga urafiki na wanaume wengine, anayependa kufuatilia maisha ya couples nyingine na kujifananisha nao, anayetamani vitu vikubwa vikubwa wakati anakuona unajitafuta!

8. Epuka kuwa na mahusiano na mwanamke anayeona anakupa favour kuwa na wewe, anayeona uzuri wake ama show zake kitandani ndiyo kila kitu!

9. Epuka kuwa na mwanamke anayeona wewe siyo saizi yake sema basi tu, asiyeweza kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake, asiyejivunia kuwa na wewe, asiyeweza kwenda out na wewe! Epuka huyo!

10. Epuka mwanamke mwenye password nyingi sana kwenye simu yake, anayesevu namba za wanaume kwa codes, asiyeweza kupokea simu mbele yako, anayeweka airplane mode mbele yako, anayezima data mbele yako, anayeanzisha biashara bila wewe kujua mipango yake, anayependa sana kujiremba hadi kupitiliza! Epuka huyo! #HK #Fighter #NjeYaBox

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents