FahamuMakala

Je, Unaijua sababu ya Gari za Shule kupakwa rangi za njano??

Si jambo la kushangaza kama ukitembelea mataifa mbalimbali na kukuta magari ya kubebea wanafunzi (School Bus) yakawa na rangi ya kufanana, yaani rangi ya njano. Fahamu kuwa rangi hiyo kwenye mabasi ya smule iliidhinishwa April Mwaka 1939 na mtaalamu wa elimu aliyefahamika kwa mina Frank W. Cyr.

Sababu kubwa ikiwa njano inaonekana kwa urahisi zaidi gizani na hii ndiyo moja ya sababu kuu kuchaguliwa kutumiwa kwenye magari ya shule, huku lengo likiwa kulinda Usalama wa Wanafunzi usiku au mchana kwa kuonekana haraka zaidi na kuepusha ajali.

Sababu ya pili kuwekwa kwa rangi ya njano na maandishi meusi ni kufuatiwa na giza la asubuhi hivyo rangi hiyo na maandishi yake itamsaidia mwanafunzi kuona basi hilo kwa haraka zaidi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents