Promotion

Vodacom yazindua huduma mpya ya ‘Simu Dokta’

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya itakayowawezesha watumiaji wa mtandao wa kampuni hiyo kupata taarifa muhimu kuhusu afya kwa siku 30 mfululizo bila malipo.

001.SIMU DOKTA
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mwili Mzima wa Binadamu,Meshack Shimwela(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuzindua huduma mpya ya”Simu Dokta”itakayowawezesha wateja wanaotumia mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom kupata huduma hiyo bure jinsi ya kujiunga mteja anatakiwa kutuma neno DAKTARI kwenda namba 15542 na Katikati ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na watoto,Sulende Kubhoja

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Simu Dokta, Dk Meshack Shimwela ambaye ni Bingwa wa magonjwa ya mwili wa binadamu alisema upatikanaji wa taarifa sahihi za kiafya ni moja kati ya hatua muhimu za kupambana na magonjwa mbali mbali.

Dk Shimwela alisema huduma hiyo itatoa mchango mkubwa katika kuuhabarisha umma juu ya masuala muhimu ya kiafya na kuongeza kuwa ujumbe wa mara kwa mara utawakumbusha watu na namna ya kujikinga pamoja na kuchukua hatua sahihi juu ya magonjwa. Shimwela aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuzindua huduma hiyo kwa ajili ya umma na kusema kuwa inaendena na Malengo ya Milenia haswa namba sita linalosisitiza kupambana na maogonjwa mbali mbali akiwataka Watanzania kuitumia huduma hiyo ambayo ni muhimu kwa kila mtu.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa alisema taarifa hizo zitakuwa katika mfumo wa ujumbe mfupi wa maneno (sms) na mteja atakuwa akizipata kila siku kupitia simu yake ya mkononi bure kwa mwezi baada ya kujisajili kwa kutuma neno DAKTARI kwenda 15542.

“Lengo la huduma hii ni kuchochea na kusaidia wananchi kujua mambo mbalimbali ya kiafya ambayo wamekuwa hawayajui au kuwa na taarifa zisizo sahihi. Taarifa hizo zitakuwa zikiandaliwa na madaktari bingwa nchini wa magonjwa mbalimbali ambao wamejitolea kuelimisha jamii.

Huduma hii itakuwa ya msaada mkubwa kwa wananchi kwani itaongeza ufahamu wa mambo mbalimbali ya kiafya na hivyo kusaidia ustawi wa jamii kwa kuwa na jamii yenye uelewa mkubwa wa mambo ya afya na kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi. Hii itakuwa ni huduma ya kwanza ya aina yake kutolewa na Vodacom ikiwahusisha madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ambao wamejitolea kuelimisha jamii ambayo inahitaji taarifa kila siku za kuwasaidia kujiepusha na maradhi au kutoa ahueni kwa magonjwa yanayowasumbua.,” alisema

Madaktari hao na taaluma za kwenye mabano ni pamoja na Dk. Meshack Shimwela (Bingwa wa Mwili wa Mwanadamu, Physician) Dk. Sulende Kubhoja (Bingwa wa watoto na moyo (Paediatrician & Cardiologist)). Dk. Munawar Kaguta, (Bingwa magonjwa ya wanawake /wajawazito (OBST/Gynecologist)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents