Siasa

Wabunge walioteuliwa jana na Rais walivyoapishwa leo Bungeni Dodoma (+ Video)

Wabunge walioteuliwa na Rais Samia Suluhu hapo jana leo wamekula viapo vyao bungeni Dodoma, nchini Tanzania.

Miongoni mwao ni Dkt Bashiru Ally ambaye alikuwa Katibu mkuu Kiongozi pamoja na Balozi Liberata Mulamula ambae ndio Waziri wa mambo ya nje wa sasa.

Muda mfupi baadae mawaziri walioteuliwa watakula kiapo mbele ya Rais Samia huko Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Hapo jana Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan alitaja baraza jipya la mawaziri wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango.

Na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Balozi Hussein Yahya Katanga kuteuliwa kushika nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents