Habari

Wafanyakazi wa SBL waungana na umma kusafisha mto Mirongo siku ya maji

Katika kuadhimishaSiku ya Maji Duniani, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imesisitiza dhamira yake katika mipango ya utoaji wa maji safi nasalama kwenye jamii za watanzania pamoja na kulinda vyanzovya maji, huku wafanyakazi wake wakiungana na watanzaniakufanya usafi mto Mirongo jijini unaopeleka maji yake ZiwaVictoria jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika jana, Meneja waMawasiliano na Mambo Endelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisemakampuni hiyo iko tayari kuendelea kuwekeza kwenye juhudi zakulinda vyanzo vya maji sawa sawa na kauli mbiu ya mwaka huu. Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya maji duniani ni kuongezamabadiliko kupata suluhisho la mgogoro wa maji safi.

Mto Mirongo unaopita jijini Mwanza ni mchafu sana na mara nyingine wakazi wa eneo hilo hulaumiwa kwa kutupa uchafukwenye mto huo hasa hasa wakati wa mvua, kitu ambachokinaweza kuathiri afya zao na kusababisha magonjwa kamakipindupindu. Zoezi la usafi wa mto huo lilifanya nawafanyakazi wa SBL kwa kushirikiana na Bodi ya Maji yaBonde la Ziwa Victoria.

Hatibu alisema SBL imefanikisha mambo mengiyanayohusiana na huduma za maji na utunzaji wake ikiwemomiradi mikubwa 24 ya maji nchini ndani ya miaka kumiiliyopita ambapo miradi hiyo kwa pamoja imenufaisha watumilioni 2 na maji safi na bure kupitia programu yakeijulikanayo kama ‘Water of Life’.

“SBL itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuwezeshajamii zenye uhitaji wa maji safi na salama kupata maji. Hii niahadi tuliyojiwekea chini ya mpango kazi wetu tunaouitaSociety 2030,” alisema.

Mapema mwezi huu, SBL iliwekeza jumla ya Tsh milioni 380 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa bwawa la maji la Kwamiziwilayani Handeni, mkoani Tanga. Baada ya kukamilika mradihuo unatarajiwa kunufaisha maelfu ya wakazi katika wilaya hiyo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents