Habari

Wanaotaka ushoga watafute nchi yao – Mwigulu Nchemba (+Video)

Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba amesema watu wanaotaka haki za ushoga watafute nchi ya kwenda ambayo itatoa haki hiyo lakini si Tanzania.

Waziri wa Mambo ya ndani Mh Mwigulu Nchemba

Waziri Nchemba amesema kama kuna taasisi yoyote imesajiliwa nchini na inafanya kampeni za haki za ushoga basi atafuta usajili huo na watu wake kukamata na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Wanaotaka haki za ushoga watafute tu nchi yao nyingine ambayo inaruhusu mambo hayo wakakae huko, kama ni taasisi imesajiliwa kwenye nchi yetu tukaigundua inafanya kampeni ya haki hizo na bahati nzuri zinasajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani nitazifutia usajili wao…

…..na kama ni raia wa Tanzania anaendesha kampeni hizo tutamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria, na kama si raia amekuja kwenye nchi yetu kuja kuendesha haki hizo tutampa amri ya kuondoka ndani ya nchi yetu hatapata fursa hata ya kuchomoa chaji ya simu kwenye soketi ya umeme” amesema Nchemba.

https://youtu.be/OnxtzAKTHe0

Kwa upande mwingine Waziri Nchemba amemuunga mkono kauli ya Rais Magufuli dhidi ya wanafunzi ambao watapata ujauzito wakiwa shuleni na kusema watu wanaopinga jambo hilo wasitumie nguvu kubwa kupinga bali wajenge shule zao wao watoe hiyo haki ya kusomesha wanafunzi wajawazito au wale ambao tayari wamejifungua na siyo kulazimisha serikali kufanya hayo.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents