AfyaHabari

Wanaozaa Watoto Njiti kunufaika

Wanawake wafanyakazi wanaojifungua watoto Njiti wanasema siku 84 zilizowekwa kisheria kama likizo ya uzazi hazitoshelezi kulea watoto hao, wakiomba kufanyika marekebisho ya sheria ili kuwaongezea muda.

Wakati wakipokea msaada wa vifaa vya usafi vilivyotolewa na idara ya wanawake ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikalini na Afya Tanzania (Tughe) waliotembelea Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi leo Machi 6, 2024.

“Siku 80 ni chache kumuacha mtoto njiti na kuanza kazi, kwani anakuwa hajatengemaa vizuri. Ni veema iwekwe sheria ambayo inatambua kulipiza miezi inayotimiza kipindi cha kujifungua kama mjamzito amejmifungua ndani ya miesi saba basi linizzo yak ijumuishwe miei mitatu na siku 80, “ amesema Felister Assenga ambaye ni ofisa muuguzi kwenye hospitali ya Tumbi.

Amesema kuwa wanawake wanaojifungua watoto njiti wakiongezewa muda wa likizo, watatekeleza majukumu yao kwa ufanisi, pindi wanaporejea kazini kwa kuwa hawatakuwa na mawazo mengi kichwani kwa kuwaza watoto wao.

Kwa épande wake, Sikitu Salumu amble pia ni miongoni mua wanawake waliojifungua watoto njiti ndani ya hospitali ya Tumbi, amesema kuwa malezi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, yanahitaji nafasi na muda wa kutosha hivyo kuna kila sababu ya jamii kulitambua hilo ili kutoa ushirikiano.

“Natoa wito kwa jamii kuna baadhi wamekuwa wakihusisha na imani potofu pindi mwanamke anapojifungua mtoto njiti, jambo ambalo sio kweli ni lazima  watambua kuwa kila kitu kinapangwa na Mungu, hivyo tunapaswa tuwapende watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na si kuwawazia vibaya,”

Akizungumza baada ya kukabidhi masada huo ambao ni vifaa via usafi na nguo za kusitiri watoto wachanga, Ofisa Elimu Kazi wa Tughe makao makuu, Nsubisi Mwasendede amesema chama hicho kinaiomba Serikali kufanya maboresho katika sheria zake, ili kuwaongezea siku za likizo ya uzazi wafanyakazi wanawake wanajifungua watoto njiti.

“Sheria ya sasa ya ajira na mahusiano kazını imekuwa ikitoa siku 84 kwa wanawake wanaojifungua mtoto mmoja na pia siku 100 kwa wanaojifungua zaidi ya mtoto mmoja wala hadisemi chochote kuhusu wanawake wanaojifungua watoto njiti.

“Ndio mana tumeona ni vyema kuikumbusha Serikali kufanya mabadiliko ili kuwaongezea muda wanawake hao,”

Likizo watoto njiti Bungeni;

Suala hilo la likizo liliwahi kuibuliwa bungeni jijini Dodoma Juni 25, 2019 ambapo aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi na Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala bora), Mary Mwanjelwa alisema kuwa Serikali imeweka utaratibu kuwa mtumishi wa umma anayejifungua pacha zaidi ya wawili au watoto njiti.

Alisema mwajiri wake anapaswa kuwasilisha hoja kwa katibu Mkuu (Utumishi) ili kupata kibali cha kuongezewa muda wa likizo.

“Ikitokea mtumishi wa Umma kajifungua watoto pacha zaidi ya wawili au watoto njiti na kulazimika kuwa na muda zaidi wa kuhudumia watoto hao, mwajiri wake anapaswa kuwasiliana na katibu Mkuu (Utumishi) ili atoe kibali cha kuongezewa muda wa likizo ya Uzazi”;.

Ziara ya TUGHE

Naye Mwenyekiti wa idara ya wanawake (TUGHE) makao makuu Agnes Ngereza, amesema katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani, wameona ni vema kuwatembelea na kutoa msaada kwenye wodi ya wanawake waliojifungua watoto njiti na kupata changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuziwasilisha kwa wadau wengine.

Kwa upande wake, Muuguzi Bingwa wa watoto hospitalini hapo, Maua Pendo ameushukuru Uongozi wa TUGHE kwa kutoa msaada huo kwa wanawake na kuziomba taasisi zingine kuiga mfano huo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

CHANZO: MWANANCHI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents