Habari

Wanasayansi Australia wagundua namna ya kupambana na Corona, wengine wapona

Wanasayansi nchini Australia wamesema kuwa wamegundua namna gani mfumo wa kinga mwilini unaweza kupambana na virusi vya Covid-19.

    Watafiti wakionesha namna ambavyo mfumo wa kinga unavyopambana na virusi

Utafiti wao, uliochapishwa kwenye jarida la Nature siku ya Jumanne, unaonesha kuwa watu wanapona maambukizi ya virusi, kama ambavyo wanavyopona mafua.

Duniani kote, mamlaka zimethibitisha maambukizi kwa zaidi ya watu 160,000 ya virusi vya corona na vifo karibu 6,500.

”Ugunduzi huu ni muhimu kwasababu ni mara ya kwanza ambapo tunafahamishwa namna ambavyo kinga zetu zinavyopambana na virusi vya corona,” amesema mwandishi mwenza Profesa Katherine Kedzierska.

Taasisi ya utafiti ya magonjwa ya maambukizi na kinga ya Peter Doherty wa Melbourne amesifiwa na wataalamu wengine, mmoja akieleza kuwa ni ”mafanikio mapya”.

Kilichobainika

Watu wengi wamepona virusi vya Covid-19, ikimaanisha kuwa tayari ilijulikana kuwa mfumo wa kinga unaweza kupambana na virusi.

Lakini kwa mara ya kwanza, utafiti ulibaini aina nne za seli za kinga ambazo zinaweza kupambana na Covid-19.

Zilichunguzwa kwa kumfuatilia mgonjwa ambaye alikuwa na maambukizi ya virusi lakini ambaye hakuwa na matatizo ya kiafya hapo awali.

Mwanamke mmoja mwenye miaka 47 kutoka mjini Wuhan, China aliyewasili hospitali nchini Australia. Alipona ndani ya siku 14.

Kwa mujibu wa BBC, Profesa Kedzierska ameiambia BBC kuwa timu yake imechunguza ”uwezo wa kinga kupambana na virusi” kwa mgonjwa huu.

Siku tatu kabla mwanamke mmoja alianza kujisikia vizuri, seli zilioonekana kwenye mfumo wa damu. Katika wagonjwa wa maradhi ya mfumo wa upumuaji, seli hizi pia zinaonekana kabla ya kupona, Profesa Kedzierska alieleza.Picha ya mapafu ya mgonjwa siku ya tano (kushoto) na (kulia) ikionesha yakiwa yamepona siku kumiPicha inayoonesha mapafu yakiwa yameanza kupona baada ya seli za kinga kuonekana

”Tulifurahia matokeo yetu-na ukweli kuwa tunaweza kuona seli za kinga kwa mtu aliyegundulika, kabla ya afya yake kuimarika,” aliiambia BBC.

Wanasayansi walifanya uchunguzi wao kwa wiki nne ili kutathimini hilo, aliongeza.

Hatua hii imesaidia nini?

Kubaini wakati seli za kinga zinaingia zinaweza kusaidia “kutabiri mwenendo wa virusi”, alisema Prof Bruce Thompson, Mkuu wa kitivo cha sayansi ya afya katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Swinburne.

Waziri wa Afya wa Australia Greg Hunt alisema kupatikana pia kunaweza kusaidia “kufuatilia kwa haraka” chanjo na tiba inayowezekana kwa wagonjwa walioambukizwa.

Prof Kedzierska alisema hatua inayofuata kwa wanasayansi ni kutazama kwa nini kinga ni dhaifu kwa wagonjwa walio katika hali mbaya.

“Ni muhimu sana sasa kuelewa ni nini kinachopungua au tofauti kwa wagonjwa ambao wamekufa au ambao wana ugonjwa ulio katika hali mbaya – kwa hivyo tunaweza kuelewa jinsi ya kuwalinda,” alisema.

Mnamo Januari, taasisi hiyo ikawa ya kwanza ulimwenguni kuunda tena virusi nje ya Uchina.

Kituo hicho kimepokea fedha zaidi kutoka kwa serikali ya Australia na pia michango kutoka kwa wafanyabiashara na bilionea wa Kichina Jack Ma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents