Afya

Wanaume wanaoshiriki mapenzi kwa njia ya mdomo wapo hatarini kiafya kuliko wanawake

Kama wewe ni mwanamme na huwa unashiriki mapenzi na mkeo au mchumba wako kwa njia ya mdomo ‘Oral Sex’ basi acha tabia hiyo mara moja kwani sio salama kwa afya yako na endapo utaendelea basi huenda ukapatwa na saratani ya koo.

Tokeo la picha la Oral sex

Kwa mujibu wa tafiti mpya zilizofanywa na chuo cha afya cha Johns Hopkins zinaonesha kuwa Wanaume ambao wameshashiriki mara kwa mara mapenzi na wanawake tofauti tofauti kwa njia ya mdomo basi wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya koo.

Tafiti hizo zimeonesha kuwa wanaume wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya saratani ya koo kuliko wanawake wanaoshiriki aina hiyo ya mapenzi kutokana na ongezeko kubwa la virusi vya papilloma duniani.

Kwenye utafiti huo umeeleza kuwa kwa sasa wanaume wengi duniani wanauhitaji kupata kinga ya virusi vya papilloma ambavyo huenezwa kwa njia ya ngono ili kuzuia ongezeko hilo kwa kizazi kijacho.

Kesi za ugonjwa wa saratani ya koo kwa wanaume zinaelezwa kuongezeka duniani kila mwaka na utafiti huo umebaini kuwa mpaka kufikia mwaka 2020 wagonjwa wa saratani ya kizazi kwa wanawake watakuwa wachache kuliko wagonjwa wa kansa ya koo.

Hata hivyo, utafiti huo umeeleza kuwa wanaume wanaotumia singara na kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ndio wapo hatarini zaidi kupata kansa ya koo.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents