Afya

140 wapindikizwa Magoti na Nyonga Mloganzila

Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila imefanya upasuaji wa kupandikiza magoti na nyonga bandia kwa wagonjwa 140 kuanzia Novemba 2023 hadi April mwaka huu ambapo walifanikiwa kupandikiza nyonga 40 na magoti 100.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali hiyo Dkt. Godlove Mfuko ametoa taarifa hiyo wakati akielezea namna Idara ya mifupa na Ajali ilivyoisaidia jamii kupata huduma za matibabu.

Amesema idara hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo kurekebisha mifupa iliyovunjika, paja na huduma zingine za kibobezi ikiwemo upasuaji wa kiuno na upasuaji wa Mgongo.

Mgonjwa akifanyiwa upasuaji anaruhusiwa katika kipindi cha siku tatu hadi tano kulingana na aina ya upasuaji aliofanyiwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents