Burudani

Wasanii sita ambao nyimbo zao zimewapa ‘mchongo’ wa tangazo

1. Ambwene Yesaya aka AY

Ilikuwa ni mwaka 2007 ambapo mapacha wa kimuziki wa siku nyingi MwanaFA na AY waliunganisha tena nguvu ya pamoja ili kuangusha ‘bombshell’ kwenye kiwanda cha muziki nchini. Wakiwa chini ya uchawi wa Hermy B kwenye production, wasanii hao ambao juzi tu wametoka kwa Madiba kuperform kwenye Big Brother Africa, AY na MwanaFA waliachia ‘club banger iitwayo ‘Habari ndo hiyo’ ambayo ikaja kugeuka kama wimbo wa taifa mjini. Ikawa kila mtu akiutumia usemi huo baada ya kusema jambo, ‘habari ndo hiyo’. Mtandao wa Vodacom ukaona upitie hapo hapo. Uliamua kuichukua idea hiyo na kuibadilisha kidogo na kuwa ‘Habari ndo hii’ na kuitumia kwenye kampeni yake. Mtandao huo wa simu ulimpa AY kiasi ambacho miaka hiyo radio mbao zilisema alipata deal ya milioni 100 na ushee kufanya matangazo ya radio, TV, magazeti na billboards.

2. Dully Sykes

Mzee wa misifa mwaka jana zali lilimwangukia pia. Kwa mujibu wa story za mtaani ni kwamba pindi alipoachia wimbo wake uitwao ‘Bongo Flava’ kampuni ya Tigo iliutumia wimbo huu kama ring back tone bila ruhusa yake. Dully kuusikia aliamua kuwafungia breki kuwauliza kunani! Mbona anasikia wimbo wake kwenye simu lakini hela hajapewa! Jamaa akatishia kuwashtaki ndipo wakaamua kumpoza kwa kumlipa kiasi cha shilingi milioni 70 kutengeneza matangazo ya mtandao huo kwa kutumia wimbo wake. Fedha hizo na zingine anazopata kwa show za hapa na pale ndizo zimemfanya aweze kufungua studio mpya ambayo inasemekana ni miongoni mwa studio kali na ya kisasa zaidi jijini Dar es Salaam. Studio iliyopo maeneo ya Tabata inaitwa 4.12 (Four Point Twelve) na itakuwa ikirekodi aina zote za muziki pamoja na matangazo. Hiyo ni studio yake ya pili baada ya Dhahabu Records ambaye itaendelea kujitegemea.

3. Suma Lee

Mwaka jana hautasahaulika kamwe kwenye diary ya Sumalee. Kurudi kwake upya kuliwapa matumaini wasanii wengine kama yeye waliokuwa wamepotea sana kuwa siku zote katika maisha huwa kuna ‘second chance.’ Kinachotakiwa ni kuitumia vizuri nafasi hiyo na kutoka kimoja. Tangu atoe ‘Chungwa’ Sumalee alikuwa amejaribu mno kujitutumua lakini kila wimbo aliokuwa akiutoa uliishia kupigwa mara mbili tatu tu redioni na watu wanamsahau tena. Lakini alipotoa tu ‘Hakunaga’ akawa amepiga penyewe. Mtaani ikawa hakunaga! Hakunaga! Sumalee akarudi tena kwenye ramani na this time kwa kishindo kikubwa na kibiashara zaidi. Kampuni ya Vodacom haikulaza damu, ikamwaapproach na kufanya tangazo kwa wimbo wake lililokuwa likitangaza ofa yake ya simu katika msimu wa sikukuu za christmass na mwaka mpya.
Japo sauti yake haikutumika kwenye tangazo hilo, kampuni hiyo bila shaka ilimwacha na ‘mshiko’ mrefu ambao ulimsaidia kukamilisha mipango yake mikubwa katika maisha.

4. Ali Kiba

Mzee wa Cinderella mwaka jana kwake pia haukuwa mbaya kama kwa Izzo B. Dushelele, wimbo ambao kwa mujibu wa waenda klabu kila weekend ni kwamba iligeuka kosa la jinai kama Dj asipoucheza, na wasakataji wa rhuba wakipanga mstari mrefu mithiri ya msafara wa siafu na kuanza kuzunguka ukumbini kila walipousikia. Kampuni ya Airtel ikaamua kumtumia Ali Kiba na wimbo wake huo kutengeneza tangazo lake jipya. Kama wasanii hao wengine, naye akapata mkwanja mrefu kuongezea zingine nyingi alizozikamata kutoka kwenye project ya Airtel One 8.

5. Diamond

Kijana mwenye kismati cha kufa mtu, Diamond Platnumz anaendelea kuthibitisha kuwa wakati mwingine majina huwa yanavuta maana yake na kuathiri vitendo. Akiwa miongoni mwa wasanii wanaolipwa zaidi kwa show za ndani ya nchini, Diamond anasikika kwenye tangazo la Vodacoma akitumia beat na melody za wimbo wake ‘Nimpende nani’. Jana pia kupitia website yake ameweka picha akiwa kwenye studio ya MJ Records na producer Marco Chali wakipika tangazo jipya la Coca cola! Awamu hii sijui atatumia wimbo gani! Mawazo? Acha tusubiri jibu tutalipata soon.

5.Juma Nature

‘Every body stand up, every body stand up’ in Juma Nature’s voice! Maneno hayo utayasikia sana ukiliangalia tangazo la Vodacom Wajanja kwenye TV. Kampuni hiyo imeirudisha sauti ya msanii huyo wa Bongo Flava mwenye hits nyingi pengine kuliko wote nchini. Ukianza kutaja nyimbo zake zilizohit, the list is endless! Na sasa baada ya kupotea sana kwenye muziki mpya, mashabiki wake wanaweza kumsikia na kumwona akiwa kama Dj kwenye tangazo hilo lililotumia wimbo wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents