Burudani

Wasanii wa Bongo Muvi wameacha Sanaa wamehamia kulima matikiti na kuuza chakula – JB (Video)

Wasanii wa Bongo Muvi wameacha Sanaa wamehamia kulima matikiti na kuuza chakula - JB (Video)

Msanii wa Bongo Muvi pia akiwa muongozaji wa muvi (Producer) na mmiliki wa kapuni ya kuuza muvi ya Jerusalem film, Jacob Stephen amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na changamoto wanazozipata katika sanaa ya uigizaji huku akiwataja wasanii wa Bongo Muvi wengi wameitelekeza na sanaa na kuhamia kwenye kazi zingine,huku akidai wengi wamehamia kwenye biashara ya chakula na wengine kujiingiza kwenye ukulima wa Matikiti na mazao mengine.

Msanii huyo ameweza kufunguka hayo yote wakati anaongea na Waandishi wa  habari siku ambayo Wema alikuwa akifanya Press na kutoa maelekezo jinsi ya mashabiki zake kuweza kuiangalia Muvi yake ya D.A.D ambayo kaifanya na masanii kutoka Ghana Van Vicker.

JB aliongeza ” Sanaa ya Muvi Tanzania haithaminiwi sana ndo mana unaona wasanii wengi wanaacha sanaa na kujiingiza kwenye shughuli nyingine,na ndo mana amekuja mkombozi wa sanaa yetu” alikuwa akimaanisha kampuni ya MP TV ambayo kwa sasa inanunua muvi za Kitanzania na kuziuza katika soko la kimataifa.

Aliongeza ” Mwakani tunategemea kuanza kushuti muvi kwa kutumia Helcopter kwa sanaa yetu imekua na tayari makampuni makubwa yameamua kuithaminisha tasnia yetu ya Bongo Muvi”

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents