Burudani

Wasanii wajifunze kuimba muziki wa live kwendana na mabadiliko – Barnaba

Mwimbaji na mwandishi mahiri wa nyimbo, Barnaba amewashauri wasanii wenzake kujifunza kutumbuiza muziki wa live wanapokuwa kwenye majukwaa.

barnaba

Barnaba anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kutumia vyombo mbalimbali vya muziki na ni miongoni mwa wasanii waliolelewa na kukuzwa na nyumba ya vipaji Tanzania – THT.

Akizungumza kupitia Planet Bongo ya EA Radio, Barnaba amesema kutokana na soko la muziki linavyokwenda kuna haja kwa wasanii kujikita kufanya muziki wa band, na kwa wale ambao hawana uzoefu wajifunze.

“Mi nafikiri ni msanii mwenye ku tune tu, hapo sio suala la kumlazimisha msanii wala kumuhimiza, msanii mwenyewe mwenye akili na kutumia fikra za mawazo, na kuangalia kipi ni hela”

Aliongeza kuwa mabadiliko ya teknolojia yanaweza kuwa sababu nyingine itakayowalazimu wasanii kufikiria kufanya muziki wa live.

“Lakini kiukweli teknolojia na soko la muziki inabadilika, sasa kwa mtu mwenye focus na maono ya mbali, anaweza akaanza sasa, akajifunza na akawekeza sasa, sio lazima, kwa atakaeona inamsaidia kwenye maslahi yake you can do it na akaweza, ukiona haisaidii basi hatuwezi kumlazimisha mtu” alisema Barnaba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents