Burudani

Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tuzo za MTV ‘MAMA’ watajwa

Orodha ya wasanii watakaolishambulia jukwaa siku ya utolewaji wa tuzo za MTV Africa Music Awards KwaZulu-Natal 2015 (MAMA) inazidi kuongezeka.

mtvbase

Wasanii wa Afrika waliotajwa kuungana na kina Davido na Diamond, ni pamoja na 2Face (Nigeria), Wizkid (Nigeria) (South Africa), Black Motion (South Africa) pamoja Toofan (Togo).

Wasanii wengine wa Afrika ambao tayari wako kwenye orodha ya kutumbuiza kwenye tuzo hizo ni pamoja na Yemi Alade (Nigeria), Cassper Nyovest (South Africa) na Brucie (South Africa).

Kutoka Marekani atakuwepo Ne-Yo, rapper Young Thug, pamoja na muimbaji wa R&B JHENÉ AIKO.

Tuzo za MAMA zitatolewa July 18, 2015 Durban, Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents