Habari

Watakaotumia Kiingereza kulipishwa faini Italia

Serikali ya Italia ina mpango wa kuwalipisha faini Waitaliano wote watakaotumia maneno ya Kiingereza au lugha nyingine yoyote ya kigeni katika mawasiliano au nyaraka rasmi.

Sheria hiyo itawataka watu wote wanaofanya kazi kwenye utawala wa umma kuwa na uwezo wa kusoma, kuandika na kukimudu Kiitaliano.

Wale watakaoenda kinyume na sheria hiyo watalipa faini ambayo inaweza kufikia kiasi cha euro 100,000.

Pamoja na kuwa mpango huo unajumuisha lugha zote za kigeni, hata hivyo unailenga zaidi lugha ya Kiingereza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama cha Brothers of Italy ambao ndio waanzilishi wa muswada huo, matumizi ya maneno ya Kiingereza yanakidhalilisha na kukishushia hadhi kiitaliano.

Mswada huo utapelekwa Bungeni kwa majadiliano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents