BurudaniVideos

Watambue mastaa wenye vipaji vya soka na muziki duniani

Huwa tunaona Wachezaji wakiwa wanashuka kwenye mabasi yao kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa ajili ya kuingia uwanjani kucheza mechi wakiwa wamevaa Earphones/Headphones masikioni mwao. Hiyo ina maana ya kwamba wanasikiliza muziki ili kuwapa hali ya morali na furaha kabla ya kuingia uwanjani na kuwaondolea mawazo ambayo huenda yakawasumbua kisaikolojia kuelekea mchezoni.
Hata bosi mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte analitambua hilo na ameweza kuwakataza wachezaji wake kula ketchup and pizza lakini hajawazuia kusikiliza muziki.

Michezo

Bosi huyo anakiri huwa anapenda sana muziki hasa wenye maadhi ya disko ukipigwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Hivyo hivyo pia beki wa zamani wa klabu ya Manchester United,Patrice Evra alikuwa akisifika kwa kupiga muziki vizuri wakiwa katika chumba cha kubadilishia nguo na walimbatiza jina la ‘ Dj wa Manchester United.’

Hivyo wanasoka wengi tu ambao ni wapenzi wa muziki na vile vile kuna wanamuziki wengi pia ni wapenzi wa mpira wa miguu. Mfano wa wanamuziki ambao ni wapenzi wa mpira wa miguu ni rapa Snoop Dogg.

Desemba 9 mwaka 2007 wakati Watanzania tulivyokuwa tunasherekea kutimiza miaka 46 tangu nchi yetu kupata Uhuru mwaka 1961,aliyekuwa mchezaji wa klabu za Manchester United,Real Madrid,AC Milan,La Galaxy na PSG, David Beckham, alikubali mwaliko wa rapa huyo kwenda nyumbani kwake katika mji wa Los Angeles kuwafundisha mpira watoto wa wawili wa kiume Corde,22 na Cordell,19 pamoja na binti yake Cori,17.

Moja ya mafunzo waliyoyapata kutoka kwa kapteni huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ni pamoja na jinsi ya upigaji wa mipira ya adhabu na mbinu za kukokota mpira. Fani hizi zimekuwa zikiishi sambamba,hivyo kuna baadhi ya mastaa duniani ambao wamejaaliwa vipaji vyote viwili yaani mpira wa miguu na muziki. Leo tutawaangalia mastaa watano duniani wenye vipaji vya muziki na mpira wa miguu.

1. Ryan Babel

babel1new1

Mnamo tarehe 19, Desemba 1986 katika mji mkuu wa Uholanzi,Amsterdam alizaliwa rapa na mchezaji wa mpira wa miguu anayeitwa Ryan Babel aliyewahi kutamba katika vilabu vya Ajax,Liverpool,1899 Hoffenheim na Kasımpaşa.

Kwa sasa anaitumikia klabu ya soka ya Al Ain iliyopo katika falme za Kiarabu. Mshambuliaji huyu wa kidachi anasifika kwa kuweza kucheza katika nafasi tofauti za eneo la ushambuliaji,anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati au mshambuliaji wa pembeni.

Hiyo ndiyo ilikuwa moja ya sababu iliyomshawishi kocha wa timu ya taifa ya uholanzi wa wakati huo Marco van Basten kumjumuisha katika kikosi cha kwanza kilicho shiriki michuano ya kombe la dunia la mwaka 2006 katika ardhi ya Ujerumani japokuwa alikuwa na majeraha ya goti. Ryan Babel anayefahamika kama ‘ Rio ‘ kwa jina la kisanii ni mmiliki wa lebo ya muziki inayojulikana kama ‘ Space Trak Entertainment. ‘ Vile vile Rio ana studio yake ya nyumbani ambayo huwa anaitumia katika kazi zake za kisanii. Rio anasifika katika kutengeneza nyimbo zilizotamba nchini mwao kwa uwezo wake wa kurap ambapo moja ya nyimbo zake ‘ Eeyeeyo ‘ iliweza kushika namba moja kwenye chati za nchini humo.

Ryan Babel alizipokea habari hizo kwa furaha na alikaririwa akisema ‘ muziki umekuwa ni moja ya sehemu muhimu katika maisha yangu ‘.Kwa uwezo wake mkubwa wa kurap uliweza kumshawishi rapa wa kimataifa kutoka Uingereza Sway kumshirikisha katika wimbo wake na alisema kuwa Ryan Babel ni moja kati ya marapa wakali wenye ladha iliyochanganyika ya nchi mbili Uingereza na Uholanzi.

2. John Barnes

John-Barnes1

John Barnes,53 ni mzaliwa wa Kingston,Jamaica ni mtoto wa aliyekuwa kanali wa jeshi la Jamaica na kapteni wa zamani wa timu ya taifa ya Jamaica. John Barnes alichukuwa uraia wa Uingereza baada ya kuhamia nchini humo na familia yake kutoka Jamaica akiwa na umri wa miaka 12.

John Barnes alifanikiwa kurithi moja ya kazi ya baba yake ya uchezaji wa mpira wa mguu hadi alipostaafu soka la kulipwa mwaka 1999. Alimalizia maisha yake ya soka katika klabu ya Charlton Athletic ya Uingereza. Kabla ya hapo alitamba katika vilabu vya Watford,Newcastle United, Liverpool pamoja na Sudbury Court ambayo ndiyo klabu aliyoanzia maisha yake ya soka mwaka 1980.
John Barnes alikuwa winga mwenye tuzo mbili za Chama cha Soka cha wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza kama mchezaji bora wa mwaka.

https://www.youtube.com/watch?v=e1KQNUecm2o

Katika nyanja za muziki John Barnes ana uwezo wa kurap pamoja na kuimba/. taa huyu atakumbukwa katika ushiriki wake wa moja ya wimbo mkubwa kabisa kuwahi kutokea nchini uingereza “World in Motion” alioshirikishwa na kikundi kinachoitwa “New World” na ulikuwa wimbo maalumu kabisa kwa ajili ya kuwapa nguvu wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza waliokuwa katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1990 ambao ulifanya vizuri na ulishika namba moja katika chati za muziki za nchini Uingereza.

3. Hussein Machozi

13774384_907556532707346_1837129448_n

Hussein Machozi ni Msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania anayeiwakilisha kanda ya ziwa. Mbali na kipaji chake cha kuimba pia amejaaliwa kipaji cha kucheza soka na aliwahi kucheza soka katika klabu ya Kagera Sugar kabla ya kujikitika katika bongo fleva ambapo aliachana na klabu hiyo baada ya kutofautiana na locha na uongozi wa timu hiyo.

Staa huyu mwenye albamu mbili alizungumza na mtandao wa globalpublishers.co.tz na kuelezea moja ya tukio ambalo hawezi kulisahau wakati akicheza mpira ambapo alidhaniwa kuwa amepoteza maisha. Machozi alisema, “kuna siku nikiwa mkoani Kagera katika uwanja wa mazoezi wa Kagera, wakati huo nilikuwa nikiichezea Kagera Sugar B,tulikuwa tunafanya mazoezi, kama kawaida, ikatokea kona, katika harakati za kuupiga mpira nikagongwa sehemu ya nyuma ya kichwa na mwenzangu, basi palepale nilipoteza fahamu na kuanza kutoka damu puani, masikioni na mdomoni.”

“Kwa jinsi nilivyosimuliwa,ni kuwa baada ya tukio lile nilikimbizwa hospitali ya Kihaka muda huohuo huku wengi wakiamini kuwa labda nimefariki,nilipofikishwa hospitalini, daktari aliyenipokea naye aliamini nimeshapoteza maisha akalipitisha hilo kuwa nimeshafariki dunia. Zikaanza taratibu za mwili wangu kupelekwa mochwari, wakati hayo yanafanyika mimi sikuwa na fahamu kabisa nikiwa nimefikishwa eneo la tukio na tayari nimewekwa pamba masikioni na puani,hapo nikawa nasubiri nichomwe sindano kabla ya mwili wangu kuhifadhiwa.

“Kabla sijachomwa sindano, ghafla nilishtuka na kujikuta nipo sehemu ambayo sijielewi, basi nikaanza kutoa zile pamba ambazo zilikuwa puani na masikioni. Wakati naendelea na zoezi hilo, akili ilikuwa haijakaa sawa, kile chumba nilimowekwa aliingia nesi akiwa na vifaa vyake, ile kuniona vile tu akaanza kukimbia,mimi pia nikatoka nduki,hapo akili ilikuwa haipo kabisa,nikawa nakimbia na yule nesi naye akawa anakimbia mpaka tukatoka nje huku nikiwa bado sijielewi,” alisimulia.

“Hatua kadhaa mbele nilimuona mama fulani sijui alikuwa nesi yule,hata sikumbuki vizuri,akatoa kanga anifunike kwa kuwa nilikuwa mtupu, sikumjali.Akatokea rafiki yangu mmoja akaniambia kuwa sijavaa nguo, ndiyo nikashtuka na hapo ndipo akili zikawa kama zimerudi ghafla.” Hussein Machozi alimaliza kwa kusema “Nikafunikwa palepale na ile kanga,cha kwanza kabisa nikaomba simu nimpigie mama yangu maana naye alijua tayari nimefariki, nyumbani walianza kuweka msiba wangu. Ajabu yule daktari aliyethibitisha nimefariki alitoweka pale hospitali na mpaka leo hii haijulikani yuko wapi”.

Kwa sasa staa huyu aliyewahi kung’ara na nyimbo zake za Kafia Gheto,Utaipenda, Full Shangwe, anajiandaa kurudi katika ligi kuu ya Tanzania Bara ya msimu huu 2016/2017 kwa kurudi tena kuichezea klabu yake ya zamani ya Kagera Sugar.

4. Memphis Depay

Memphis-Depay-610683

Memphis Depay,22 ni mshambuliaji anayekipiga katika klabu ya Manchester United. Ni moja kati ya wachezaji vijana wanaotabiriwa makubwa ya kuja kuwa moja ya wachezaji bora duniani. Kocha wa zamani wa Manchester United, Louis Van Gaal anaamini Memphis Depay ni mchezaji atakayekuja kuwa moja ya washambuliaji bora duniani ndio maana akamnunua winga huyo wa Kiholanzi kutoka club ya PSV Eindhoven na kuongeza nguvu katika klabu hiyo.

https://www.youtube.com/watch?v=DtYaNhNiBd0

Licha ya uwezo wake uwanjani anaosifika wa kukokota mpira na kupiga mashuti ya mbali pia ana uwezo mkubwa wa kurap kwa lugha ya kidachi.Mwaka 2014 kulikuwa na video iliyokuwa ikitambaa mitandaoni ikimuonesha winga huyo wa zamani wa PSV aki rap ambapo mashabiki wa timu ya taifa ya uholanzi na PSV wakiwa wanafananisha uwezo wake wa ku rap na rapa Lil Wayne.

5. Clint Dempsey

Kiungo huyu yupo kwenye timu ya taifa ya Marekani na lwa sasa anakipiga kwa mkopo katika klabu ya Fulham akitokea klabu ya Seattle Sounders FC ya nchini Marekani. Hii ni mara ya pili kwa Clint Dempsey kurudi katika klabu ya Fulham kwani alishaichezea klabu hiyo kuanzia mwaka 2007-2012 na kuichezea michezo 184 na kufunga mabao 50 na hiyo ndio ilimpelekea kushinda tunzo ya kuwa mchezaji bora wa klabu ya Fulham mfululizo kwa miaka yake miwili ya mwisho klabuni hapo.

Ukiachilia mbali uwezo wake mkubwa wa kupachika mabao, Dempsey,33 anajulikana pia kama ‘ Duece ‘ katika tasnia ya muziki. Siku 12 kabla ya kuanza kwa kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani,Clint Dempsey aka Duece alishirikiana na marapa kutoka Texas XO na Big Hawk na kufanya wimbo ulioandaliwa na Nike maalum kwa ajili ya kombe la Dunia.

Duece ana albamu mbili “Don’t Tread ” iliyotoka mwaka 2006 pamoja na “The Redux” yenye jumla ya track 13 iliyotoka mwaka 2014.

Imeandaliwa na
FARAJI FOWZ ZEGGESON
Instagram : @xfowz
Twitter : @fowzwheezy
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents