HabariUncategorized

Watanzania 6,368 watembelea hifadhi za taifa baada ya ‘OFA’ ya Tanapa

Baada ya tangazo la Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira la kutoa OFA kwa Watanzania kutembelea mbuga za wanyama bure kwa siku tatu hatimae Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) imetoa takwimu za watanzania waliotembelea hifadhi za taifa.

Picha inayohusiana

TANAPA imesema  Watanzania takribani 6,368 wametembelea hifadhi za Taifa nchini kufuatia uamuzi wa kushirikiana na Wizara ya Utalii kuruhusu watanzania kuingia kwenye hifadhi za wanyamapori nchini bila kiingilio kwa kipindi cha siku tatu kuanzia 2 – 4 Juni 2017 mwaka , kama sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.

Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Mkoani Arusha iliongoza kwa kupokea wageni 1,582  ikifuatia na hifadhi ya Serengeti mkoani Mara wageni 1,085 na mikumi mkoani Morogoro wageni 1,004.

Hifadhi nyingine zilizopokea wageni wachache ni Kitulo mkoani Mbeya wageni 13, Mkomazi mkoani Kilimanjaro na Tanga wageni  43 na Gombe, Kigoma wageni 66.

Kwa hifadhi zilizotembelewa na wageni wengi uwepo wa miundombinu mizuri hususani ya barabara zinazopitika muda wote nje ya hifadhi imekuwa sababu kubwa ya hifadhi hizo kutembelewa na wageni wengi, huku zile zenye changamoto ya barabara  hususani za majini kupokea wageni wachache.

Ofa hiyo iliyotolewa kuadhimisha siku ya mazingira duniani ilijumuisha msamaha wa ada ya kiingilio na ada ya magari ya abiria na ilihusu kuvinjari kwa muda wa siku moja.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents