Habari

Watu 30 wauawa msikitini

Watu 30 wamekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya mlipuko na mashambulizi ya kufyatua risasi kutekelezwa katika msikiti wa Jawadia mjini Herat nchini Afghanistan. magharibi – imesababisha vifo vya watu takriban 30 na kusababisha wengine wengi kujeruhiwa.

Msikiti ulivyoharibiwa na tukio hilo

Msemaji wa polisi katika eneo hilo amesema shambulio hilo limetekelezwa na mlipuaji wa kujitoa muhanga ambaye hajatambulika mpaka sasa.

Shambulio dhidi ya msikiti wa Jawadia limetokea saa mbili usiku jana tar 01 Agosti wakati mamia ya waumini walipokuwa wanaswali swala ya jioni na mpaka sasa hakuna kuna kundi lolote la kigaidi lililodai kutekeleza shambulizi hilo.

Taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC zinasema mlipuaji wa kujitoa muhanga alifyatua risasi ndani ya msikiti kabla ya kujilipua.

Herat, mji uliopo karibu na mpaka na Iran, unatazamwa kuwa ni moja ya miji yenye amani nchini Afghanistan.

Mwaka jana kundi la Islamic State lililenga kutekeleza mashambulizi maeneo ya Shia katika sehemu nyingi nchini Afghanistan.

Siku ya Jumatatu kundi hilo limekiri kuhusika na shambulizi la kujitoa muhanga dhidi ya ubalozi wa Iraq katika mji mkuu Kabul.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents