Habari

Watu 38 wafariki dunia baada ya kingo za bwawa kupasuka

Watu 38 mpaka wameripotiwa kupoteza maisha huku zaidi ya familia 450 zikiyakimbia makazi yake mjini Nakuru nchini Kenya kufuatia kingo za bwawa la Patel lililopo katika eneo la Subukia kupasuka usiku wa kuamkia leo.

Kufuatia tukio hilo tayari watu 47 wamekimbizwa katika hospitali ya Nakuru/Bahati huku jitihada za uokoaji zikiendelea mjini katika eneo hilo.

Shughuli za uokoaji zikiendelea

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mjini Nakuru, Japhet Kioko amesema kuwa jitihada za kutafuta miili mingine zinaendelea kwa kutoa matope yaliyoingia kwenye makazi ya watu.

Tayari Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameshatoa salamu za rambi rambi kwa familia zilizopoteza ndugu, marafiki na jamaa kwenye tukio hilo. Soma taarifa yake iliyotolewa na Ikulu HAPA .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents