Bongo5 ExclusivesHabariSiasa

Watumishi wa Temeke wamshukuru Rais Samia, Nyongeza ya mshahara imeongeza ari ya kuchapa kazi

Baada ya serikali kutangaza kuongeza mshahara kwa 23% kwa kima cha chini, watumishi wa wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, wamesema kwamba nyongeza hiyo imewaongezea ari ya kufanya kazi kwa bidii.

Watumishi hao wa wilaya ya Temeke wameviambia vyombo vya habari kuwa nyongeza ya mshahara kwa kima cha chini, kuondolewa kwa penati ya bodi ya mikopo vimeongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii na kwamba wanaopotosha hawana nia nzuri na Taifa.

“Tunasikitishwa na wanaopotosha kwamba nyongeza ya mshahara kwa kima cha chini ni uongo, sisi watumishi tunamshukuru sana Rais Samia kwa jitihada anazozifanya kutuwekea mazingira mazuri ya kazi, nyongeza ya mshahara imetufaa sana, tumependelewa sana na serikali hii na tumehamasika kuchapa kazi,” amesema makungu Shomari, mmoja wa watumishi Temeke.

Katika hatua nyingine, watumishi hao wamesema kwamba mzigo wa kufanya kazi umezidi kupungua kwakuwa serikali imeajiri watumishi wapya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents