Habari

Waziri wa Malawi ajiua baada ya kushindwa uchaguzi

Waziri wa nchini Malawi amejiua baada ya kushindwa uchaguzi Jumanne hii na kupoteza kiti chake cha ubunge, polisi wamesema.

_75024342_75023422
Kura zikihesabiwa katika maeneo yasiyo na umeme

Naibu waziri huyo wa serikali za mitaa, Godfrey Kamanya alijipiga risasi nyumbani kwake jijini Lilongwe. Kamanya aliacha maelezo yaliyomuomba Rais Joyce Banda kuwa amlee binti yake na kumsomesha.

Hata hivyo msemaji wake amekanusha kuwa waziri huyo alijiua kutokana na kupoteza kiti cha ubunge.

Wakati huo huo matokeo ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali bado hayajatangazwa. Rais aliyepo madarakani Joyce Banda amepata upinzani mkali kutoka kwa ndugu wa rais wa kabla yake Peter Mutharika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents