Burudani

Wema Sepetu na Jokate Mwegelo waongea lugha moja kusherehekea ushindi wa Alikiba!

Ushindi wa Alikiba kwenye tuzo za KTMA 2015 haujatokana na nguvu ya Team Kiba tu bali pia nguvu ya Wema Sepetu na Jokate Mwegelo na majeshi yao.

11333662_379806792228206_1918627684_n

Alikiba na Jokate wanadaiwa kuwa na uhusiano. Wema amekuwa upande wa Kiba tangu kuachana na Diamond na wengi wamekuwa wakikichukulia kama ni kisasi.

Baada ya ushindi huo warembo hao walitumia Instagram kutoa pongezi zao.

“Hongera sana cherie @officialalikiba kwa kujishindia tuzo sita jana usiku kwenye kiba Tanzania music awards (KTMA) sorry Kilimanjaro Tanzania music awards 2015. Teh teh the,” aliandika Jokate.

“Ni kitu cha kumshukuru Mungu ulikaa kimya miaka 3 ila ukarudi na wimbo mmoja ukatuteka tena. Kusema ukweli tukiachilia mbali ushabiki ‘mwana’ ulituliza akili na ukafanya vizuri sana nchini. Mashabiki wanakupenda. Sana. Mpole hivi, mcheshi, mstaarabu. Na unajua mziki. Tunakuombea sasa hii iwe motisha ya wewe kufika mbali zaidi. Ndio kwanza safari imeanza. Uzuri unaomba mungu so najua hata kutupa. Ila kaza mwana we kazaaa!!! We are behind you,” aliongeza.

Naye Wema aliandika: Nilitaka zote saba ila hata 6 pia sio mbaya…. #KingKiba…. Umetisha.”

Jokate pia amepost picha akiwa na Wema na kuandika: It’s a beautiful and powerful thing when strong girls come together. emojiemojiemoji️. With The Sweetheart @wemasepetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents