Burudani

Wesley Snipes atoka jela lakini………

Muigizaji wa filamu za action Wesley Snipes ametoka jela wiki hii baada ya kufungwa kwa karibu miaka miwili kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

Wesley+Snipes+Overture+Films+Premiere+Brooklyn+e9Fde0FQJqtx

Muigizaji huyo alikuwa amefungwa kwenye gereza la McKean Federal Correctional Institution huko Pennsylvania.

Wesley, alifungwa December 2010 na kutoka April 2 na kupelekwa New York Community Corrections Office ambako atatumikia kifungo cha ndani – home arrest.

Baada ya July 19, nyota huyo wa Blade ataachiwa huru kabisa ili kuendelea na maisha yake ya kawaida. Staa huyo anatarajia kuwa miongoni mwa waigizaji kwenye filamu ya The Expendable 3.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents