Burudani

Wizkid aelezea jinsi Drake alivyomtafuta Instagram na kupanga kufanya remix ya ‘Ojuelegba’

Superstar wa Nigeria, Wizkid ameelezea jinsi Drake alivyomtafuta kwaajili ya kufanya remix ya hit song yake ‘Ojuelegba’.

wizdrake

Akizungumza kupitia kituo cha Empire FM cha Ghana, Wizkid amesema kuwa mawasiliano yao yalianzia Instagram baada ya Drake kumfollow, na baadae kumuomba waonane London, Uingereza ambako remix hiyo ilifanyika.

Wizkid amesema baada ya kuona Drake amemfollow aliamua kumtumia ujumbe (direct message) na kumwambia kuwa yeye (wizkid) ni shabiki mkubwa wa muziki wake, na Drake nae akamjibu kuwa hata yeye anapenda muziki wake.

“I was there and saw that Drake followed me on Instagram so I DMed him and I was like ‘Yoh, I’m a big fan of your music and he was like I like your music as well’. So we started talking and we talked about hooking up in London, so I went to London the next day and when I got there, I saw that he had already done his verse to the song, it was just funny mehn!…’…” – Wizkid.

Wizkid aliongeza kuwa siku iliyofata alienda London na alipofika alikuta Drake ameshafanya verse yake.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na jarida la FADER, Drake alisema kuwa ni heshima kubwa kwake kushiriki kwenye wimbo wa star huyo wa Afrika, Wizkid.

https://youtu.be/6poS1zBQQfU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents