Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Wizkid na Burna boy kuitikisa duania kwa kufanya show kwenye viwanja hivi vya mpira

Wasanii wawili kutoka nchini Nigeria kuvijaza viwanja viwili vikubwa katika jiji la London Uingereza, hapa nni Burna Boy na Wizkid, ambapo Buna boy atakuwa Msanii wa kwannza Afrika kufanya show katika uwanja wa klabu ya Westham Uited unaojaza watu 80,000 katika Uwanja huo unaoitwa London StadiumĀ  Uingereza mnamo Juni 3, 2023.

Uwanja huo unachukua watu 80,000 kwa matamasha tu lakini katika mashaiki wa mpira unatakiwa kuingiza watu 66,000 kwa michezo ya mpira wa miguu.

Ni moja ya viwanja vikubwa zaidi nchini Uingereza.

Lakini kwa upande wa Wizkid atakuwa Msanii wa kwanza wa Kiafrika kufanya show katika Uwanja wa klabu ya Tottenham Hotspur uliopo London pia wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 62,850 jijini London, Uingereza mnamo Julai 29.

Ni uwanja wa tatu kwa ukubwa wa soka nchini Uingereza na nyumbani kwa klabu ya Ligi Kuu, Tottenham Hotspur.

Wasanii kutoka nchini Nigeria wanaonyesha namna gani walivyo wakuwa duniani kote hasa Wizkid na Burna boy wakienndelea kuitikisa dunia kwa upande wa muziki wa Kiafrika.

Baada ya kujaza kumbi malimali kuwa duaniani (ARENAS) sasa wamehamia viwanjani.

Ikumbukwe kuwa siku za hivi karibuni Wizkid alitangaza kuwa atakuwa na tour ya kimuziki yeye na Davido, wasanii ambao walikuwa kwenye tofauti kwa muda mrefu lakini sas akufanya show pamoja wakizunguka duaniani.

Msanii gani wa Tanzania unatamani afikie level za akina Wizkid na Burna boy level za kujaza viwanja vikubwa duaiai vya mpira??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents