Habari

Woman’s Day: Khadija Mwanamboka azindua VVK Accessories, atapa deal ya ubalozi kutoka Sense International (Picha)

Jumatano hii ilikuwa ni siku ya Wanawake Duniani ambapo, Mwanamitindo nguli hapa nchini na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vitu Vya Khadija (VVK), Bi Khadija Mwanamboka aliungana na wanawake wengine jijini Dar es salaam katika kuisherehekea siku hiyo muhimu huku akizindua bidhaa yake mpya za urembo VVK Accessories.

Khadija akiwa na wageni waliojitokeza kwenye halfa hiyo

Aidha mjasiriamali huyo alitangazwa kuwa balozi wa Shirika lisilo la kiserikali la Sense International la nchini Uingereza lenye nia ya kuwasaidia watoto wenye ulemamu wa kusikia na kuona kwa pamoja waliopo hapa nchini.

Lulu akionyesha bidhaa mpya aliyonunua kutoka kwa Khadija Mwanamboka

Akiongea na katika katika hafla hiyo, Mwanamboka alisema kuwa aliamua kuwaalika marafiki zake katika siku hiyo ili kuwataarifu mpango wake mpya alioupata kupitia Shirika lisilo la kiserikali.

“Sense International ya nchini Uingereza ina nia ya kuwasaidia watoto wenye ulemamu wa kusikia na kuona kwa pamoja waliopo hapa nchini, ambapo tutaanzisha kitu kinaitwa Pendeza Kids Collection kwa kubuni mavazi mbalimbali ambayo yatauzwa katika Duka la Shirika hilo la Sense lililopo nchini Uingereza na zingine zitauwa hapa hapa nchini ili kuwasaidia watoto hao,” alisema Khadija.

Hafla ya kuisherehekea siku hiyo adhimu kwa kina mama, ilifanyika katika Ukumbi wa Kamarambezi, Seacliff jijini Dar es salaam.


Khadija akiwa na Nancy Sumari

Bosi ya shirika la Sense International nchini Tanzania


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents