Burudani

Safari ya Yamoto Band ya Marekani kwa mara ya kwanza imeiva, ziara yao kuanza Novemba

Milango ya show za kimataifa inazidi kufunguka kwa vijana wa wanne wanaounda Yamoto Band yenye maskani yake Temeke, Dar-es-salaam.

yamoto - marekani

Ile ahadi aliyoitoa mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella kupitia Bongo5 kuwa Yamoto Band wamepata mwaliko wa kwenda kuwaburudisha Watanzania na wana Afrika Mashariki waishio Marakeni imetimia.

Promota maarufu DMK ambaye amekuwa akipeleka wasanii wengi kufanya maonesho Marekani, ikiwa ni pamoja na ile show ya Ommy Dimpoz na Shilole inayotarajiwa kufanyika Septemba 5, 2015, ameshare poster ya show ya Yamoto Band itakayofanyika katika jiji la Kansas Novemba 27, 2015.

Fella amesema kuwa wakiwa huko Yamoto wanatarajiwa kufanya show katika miji mitatu. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Yamoto Band kufanya ziara nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents