HabariMichezo

Yanga msichukulie poa, Madeama sio kinyonge

Baada ya mchezo wa Yanga SC dhidi ya Al Ahly kumalizika kwa sare 1-1 katika dimba la Benjamin Mkapa na wananchi kuonesha mchezo Bora na mzuri Kwa kutoa mechi nzuri kwa Mabingwa watetezi wa kombe la ligi ya Mabingwa Afrika bila shaka hakuna mtu wa kuwalaumu zaidi ka kuwapongeza.

Nimeona baada ya mechi hizi 2 walizocheza Yanga SC mashabiki wengi wameanza kupiga mahesabu Yao mepesi maana Yanga amecheza ugenini na CR Belzoudad akapoteza na Jana kapata sare maanake ana point Moja akishika nafasi ya nne kwenye kundi lao baadhi ya Mashabiki wamesema point zao sita zipo kwa Madeama maanake tayari wamemchukulia poa wamemchukulia mnyonge hiyo tu inaongeza ugumu wa mechi.

Katika kundi hili naona zaidi mechi atazopata Yanga ugumu ni dhdi ya Madeama Moja wanacheza soka la kupiga pasi kama Yanga mbili ratiba ya mechi wanaanza Ghana alafu wanakuja kwa Mkapa timu za Afrika Kila mtu anatamba kwao Sasa ukianza Kule ukija hapa mpinzani tayari nae atakuwa amekuona ubora na madhaifu yako maanake presha kwako itakuwa juu tena ukiwa nyumbani mbele ya Mashabiki wako.

Nimeona hata mahesabu ya Meneja wa Habari na mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe mawazo yake hayatofautiani sana na mashabiki wao Mimi hii inapotokea mechi kuwa ngumu itawafanya timu kuwa na presha.

NB:Mikatakati waliyomuwekea Al Ahly ndiyo kwa kiwango hicho hicho watumie kuwekea Madeama wapo kwenye ubora wao pia.

Credit by Isayah Dede

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents