Michezo

Yanga yapigwa faini, Injinia Hersi Said apewa Onyo kali

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Januari 27, 2022 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi yafuatayo.

Mechi namba 94: Coastal Union 0 – 2 Young Africans SC, Klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi milioni moja (1000,000) kwa kosa la washabiki wake  wanaotumiwa kama walinzi wa timu, maarufu kama makomandoo, kumzuia Mratibu wa Mchezo huo, Abdul Mgude kuingia uwanjani kwa ajili ya kusimamia zoezi la uwekaji mabango ya Wadhamini.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni ya 47 (1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti  kwa klabu.

Kiongozi wa Yanga,  Hersi Said amepewa onyo kali kwa kosa la kuingia eneo la kuchezea (pitch) mara baada ya mchezo kumalizika. Onyo hili ni kwakuzingatia Kanuni ya 47 (17&60) kuhusu taratibu za mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents