BurudaniVideos

‘You are so stupid’ Mama Wema ‘amchenjia’ Soudy Brown, ni kuhusu bifu na Man Fongo (Sauti)

Ukitaka kumhoji Mama Wema Sepetu, tena kuhusiana na issue inayomhusu mwanae, jipange, lasivyo atakutoa nishai!

mama-wema

Uliza kilichomkuta Soudy Brown wa Clouds FM. Kwa ufupi kuna mgogoro mkubwa kati ya Wema Sepetu dhidi ya Christian Bella na Man Fongo kwa pamoja na unahusiana na masuala ya show ambazo ‘design’ wamezungukana na mama ameingilia kati!

Hivyo Soudy kama kawaida yake aliongea na Man Fongo kujua upande wake wa mkasa huo, lakini hiyo ilikuwa trailer tu. Picha lilianza rasmi baada ya mtangazaji huyo bingwa wa umbeya kuongea na Mama Wema.

Salam na mazungumzo ya kwanza yalikuwa ya heri tu kabla ya mama huyo kuulizwa kuhusu Man Fongo. Haya ni mazungumzo yao:

Mama Wema: Wewe ulikuwa unataka nini?
Soudy Brown: Ahh nilisikia tu kwamba anasema [Man Fongo] umemdhalilisha, umemtolea mapovu

Mama Wema: Sasa unachotaka nifanye nini?
Soudy Brown: Ah nilitaka kujua tu kama kweli mama yangu
Mama Wema: Sasa ukijua kama ni kweli, what do you want to do?
Soudy Brown: Nilitaka tu kujua kosa lake mama

Mama Wema: Halafu ukishajua kosa lake unataka kufanya nini?
Soudy Brown; Ili tukusaidie tumkanye
Mama Wema: Mwenye kutaka kujua kosa lake ni baba yake, not you, umenielewa?
Soudy Brown: Ehh

Mama Wema; Anayetaka kujua kosa lake ni baba yake sio wewe, who are you? Wewe ni nani kwa Man Fongo? Umenielewa?
Soudy Brown: Mama kwanini unasema baba yake ndio anafaa ajue?
Mama Wema: Ah you are so stupid!
Soudy Brown: Eh mamaaaa!
Mama Wema: We Soudy, naomba uwe na heshima, naomba mfuate huyo huyo akakueleze, mimi sitaki ugomvi na wewe.

Mama Wema pia hakusita kumshushia mkong’oto mtangazaji huyo. “Nitakuchukia na nitakutandika! Unanijua nitakupiga! Simuogopi mtu yeyote, nikikukuta nakupokoa na mawe, nikome. Sasa andika uone sheshe litakalokuja kukutokea.

Sikiliza majibizano hayo hapo chini.

https://www.youtube.com/watch?v=iNyXX9RlnuY&feature=youtu.be

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents