Burudani

Yvonne kufungua milango ya wasanii wa bongo mtoni

YvonneAnajulikana kwa jina la Yvonne Sangudi (20) ambaye amezaliwa nchini Liberia, akakulia na kusomea elimu yake yote kuanzia chekechea mpaka mwisho nchini Marekani ndio maana hana anachofahamu kuhusiana na bongo kwani hii imekuwa ni mara yake ya kwanza kushuka bongo na kujingaza kama msanii.

Yvonne

 

 

 

Ni kawaida kusikia kuwa msanii alianzia hapa na kwenda nje ya nchi na kukiendeleza kipaji chake ambacho ametoka nacho hapa huku akiwa tayari anajulikana kama msanii ambaye amekwenda kutafuta michongo ili atoke lakini safari hii Medani ya burudani imekutana na mtanzania asiyejua Kiswahili kabisa huku akijinadi kama “Am Tanzanian n’ American” akiwa na maana yeye ni mtanzania na mmarekani, upo hapo?

 

 

 

Anajulikana kwa jina la Yvonne Sangudi (20) ambaye amezaliwa nchini Liberia, akakulia na kusomea elimu yake yote kuanzia chekechea mpaka mwisho nchini Marekani ndio maana hana anachofahamu kuhusiana na bongo kwani hii imekuwa ni mara yake ya kwanza kushuka bongo na kujingaza kama msanii lakini mara ya kwanza alidrop ile kikawaida ambako hakukaa kabisa kwa kifupi ni mgeni sana nchini.

 

 

 

Ukifuatilia kiundani kuhusiana na asili halisi ya utanzania wa mtoto huyu unakuta kuwa washua wake ni wakazi na wazaliwa halisi wa Tanzania tena wa Mkoani Mwanza so kwa sababu hizo mtoto anakuwa ni Msukuma Mmarekani ‘Kazi Ipo’!

 

 

 

Alikutana na Mwandishi wa gazeti hili katika hotel ya Movenpick maeneo ya town na kuanza kupig nae story lakini almanusra Mwandishi wa habri hizi atoke nduki mara tu alipogundua kuwa mtoto Kiswahili hakipandi Dah ilikuwa noma mtu wangu lakini jahazi likasonga na watu wakapeta vile vile.

 

 

 

Akizungumzia kuhusiana na maisha yake ya kisanii anasema “nimeanza kujihusisha na masuala ya muziki tangu nikiwa na umri mdogo sana ambapo albamu yangu ya kwanza niliifanya nikiwa na umri wa miaka 11 lakini ilikuwa ni ya kitoto kabisa ambapo haikuwa katika mlengo wa kibiashara zaidi niilita jina langu ‘YVONNE’

 

 

 

Hivi karibuni mtoto Yvonne amekamilisha albam yake ya kwanza lakini bado anasikilizia mchongo wa kupata kampuni ambayo itasimamia kazi zake “alichosema ni kuwa hababaiki na Makampuni makubwa nachotaka kupata kampuni ambayo itanipa dau linaloweza kukidhi mahitjai yangu na si vingine nikiwa na maana I ned a gud Ofa that what I mean”

 

 

 

Ujio wa binti huyu nchini umeambatana na ujio wa kampuni mpya itakayojihusisha na kuwasaidia wanaochipukia katika masuala ya muziki na pia kuwaajiri ili wafanya muziki kama kazi na sio burudani peke yake, “Brand New Day” ndio jina la kampuni yangu ambayo nimeainzisha nikiwa Mtoni ikishirikiana na Bristol Magazine, gazeti kubwa sana nchini marekani, na hapa Home ndio nimekuja kuaianzisha rasmi na nikirudi next time nitakuwa na mikataba na kila kitu ila wawakilishi na kila kitu wapo hapa nimeshawapata na wanajua nini cha kufanya ili kufanikisha malengo haya”-Yvonne.

 

 

 

Pamoja na hayo yote Yvonne amekuwa akifanya show kwenye matamasha mbali mbali zikiwemo za viongozi mbali mbali wa serikali kwa mfano alipata bahati ya kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania siku ambayo Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete alipotimba marekani, amewahi kufanya show katika hafla iliyoandaliwa na Mke wa Rais Bush wa Marekani, Pia amefanya makamuzi alipokuja Raisi wa Liberia Ellen Johnson – Sir Leaf na matamasha mengine mbali mbali nay a kawaida.

 

 

 

Mpaka sasa ndio kwaaaanza amekamilisha albam yake ya kwanza ambayo ndio inatarajiwa kuwa ni tiketi ya kufanya aingie mkataba na kampuni yoyote ambayo itasiiliza kazi zake na kumkubali kwani kwa hapa bongo hakuna mpinzani kila mtu amekiri kuwa mtoto yuko juu na anaweza kuyafikia matawi ya juu zaidi hapo baadae.

 

 

 

Albam yake inakwenda kwa jina WYCKED ambayo inanjumla ya nyimbo 17 n ndani yake amewashirikisha watu kama J Starters, NBox KB na wengine kibao lakini kazi nyingi katika Alba yake hiyo amezifanya yeye mwenyewe akiwa na Producer wake “licha ya kuwa msanii pia nina uwezo mkubwa sana wa kuandaa muziki, ninapiga Kinanda pia natumia Logic na Protools katika kuandaa ngoma zangu nikiwa na producer wangu”

 

 

 

Yvonne anaamini mafanikio huanzia nyumbani ndio sababu zilizomfanya aje kwanza kujitambulisha kwa watanzania ili ijulikane kuwa kuna mtanzania mwenzao ambaye anaiwakilisha Tanzania ile mbaya katika medani ya muziki duniani “katika vitu ambavyo naamini kabisa ni kuja kuwa benge la super star ulimwenguni, sidhani kama nafanikiwa katika hilo then nyumbani kwetu sifahamiki sio fresh”

 

 

 

Akizungumzia muziki wa kitanzania Yvonne amedai kuwa hakuna msanii ambaye anaminispire lakini kuna kazi anazizimia ikiwemo ‘sogea sogea’ ya ya Ray C, ‘Nalia’ ya PnC, ‘Sikiliza’ ya Mangwea na Lady Jay Dee, na ngoma za AY, pia amedai anazimia sana nyimbo za Kanda Bongo Man na kwa upande wa Africa anakoma ile mbaya na Hayati Brenda Fassie.

 

 

 

Kwa unyamwezini msanii wake wa kwanza ambaye anamzimia kuliko wote ni Christina Agurela then wanafata wasanii kama Bob Marley, Sean Poul, Maria Carey Sting na wengine baadhi.

 

 

 

Aliitaja baadhi ya mikono ambayo itapatikana katika albam yake ni pamoja na African Girl, Wind em Up, Giv It 2 dem akiwa ameshirikiana na J Starters, Bongo5.com ilipata fursa ya kuisikiliza baadhi ya mikono ya binti huyu na yaani unawe kuona kuwa mtoto hana safari ndefu mpaka kufikia matawi ya hatari ni kwamba soon tutaisikia habari yake.

 

 

 

Yvonne ameshatimua nchini na kuelekea New York ambapo ndipo anaishi na kufanya shughuli zake na anatarajia kuelekea jijini Holly Wood ambapo ana mkutano maalum na baadhi ya wadau, mkutano huo ukiwa ni maalum kujadili kuhusiana na albam yake na mkataba tayari kwa kuingia katika soko la muziki.

 

 

 

Alimaliza kwa kusema kuwa anawaahidi watanzania kuwa hatawaangusha na atafanya kila awezalo kuhakikisha Bongo inakuwa juu.

 

Bofya hapa kupata ujumbe fupi kutoka kwa Yvonne

 

Bofya hapa kumsikiliza Yvonne akiimba kidogo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents