Burudani

Zari alamba dili nono Afrika Kusini

Zari The Boss Lady amepata dili la kutangaza magari ya Mercedez-Benz yanayosambazwa na kampuni ya AMG Performance Centre ya nchini Afrika ya Kusini.

Kwa muda huu ukipita katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Zari ameweka picha mbali mbali akiwa katika magari hayo na kupendezesha na suti yake ya rangi ya zambarau na kuandika maneno yafuatayo;

zarithebosslady@amgperformancecentremenlyn thank you for making my day with this baby courtesy of @galston.anthonyAMG GT ROADSTER?

Dili la mrembo huyo linakuja wiki kadhaa baada ya baba watoto wake, Diamond Platnumz kupata dili la kutangaza kinywaji cha Belaire cha nchini Ufaransaa hivyo kuungana na mstaa wakubwa duniani kama Dj Khaled na Rick Ross kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents