Habari

Rais Magufuli awagusa Kituo cha Haki za Binadamu (Video)

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),wampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka wazi msimamo wake wa kutounga mkono adhabu ya kifo kwa imani yake binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es salaam, Naibu Mkurugenzi wa Utetezi(LHRC), Anna Henga amesema adhabu hiyo ni ya kinyama na isiyostahili kwa binadamu yeyote yule.

Bi Anna alisema kuwa bila kuathiri msimamo huo wa Rais Magufuli wao kama watetezi wa haki za binadamu wanazo sababu nyingine nyingi za kupinga adabu hiyo kama:

1: adhabu ya kifo ni adhabu ya kikatili isiyo na staha,inayotweza utu wa binadamu, inafanya serikali ionekane pia kama mhalifu wa kuua 2: Adhabu ya kibaguzi maana mara nyingi wanaopatikana na hatia na kupewa adhabu hii ni maskini wasioweza kuwa na uwakilishi na ushauri wa kisheria na watu wanyonge.

3: Ni vigumu kuthibitisha kuwa inatekelezwa tu kwa wale watu ambao wametenda na kukutwa na hatia ya kosa hili au wabaya zaidi 4: Adhabu hii ikitolewa kwa mtu asiyekuwa na hatia kimakosa huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na uwezekano wa kuwa na mianya ya makosa. 5:Adhabu hii haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi. Haimsaidii mtu yeyote hata familia ya muathirika.

6: Hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hii inazuia watu wengine kutokutenda makosa kama hayo 7: Mfumo wa sheria una mianya ya makosa na ni vigumu kuwa na uhakika kuwa haki inatendeka kila wakati. Wapelelezi – ubambikiwaji wa kesi, changamoto za kiupelelezi, waendesha mashtaka,huweza kufanya kosa, majaji kufungwa mikono kulingana na awakilishi mbele yao kubanwa na sheria inayowataka kutoa adhabu ya kifo kwenye makosa tajwa.

Hata hivyo kituo hicho kimeweka wazi kwamba hawakubaliani kwa namna yoyote na vitendo vya namna yoyote na vitendo vya mauaji na kwa namna hiyo hiyo wasingependa kuona muuaji anauwawa baada ya kuua huku wakieleza kuwa kufanya hivyo ni kuhalalisha kifo.

Na Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents