Habari

Ziara: Dr. Shein ataja sababu ya Wanzanzibar wengi kukosa fursa za kusoma (Picha/Video)

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein amewataka wanafunzi wa shule ya msingi Kihinani, kuhakikisha wanatuma fursa nzuri ya masomo waliyoipata na ametaja sababu ya wananchi wengi wa kisiwani humo kukosa kupata elimu ya shuleni.

Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatiwa na  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahamoud pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki  Pembe Juma

Dkt Shein amesema hayo leo katika uzinduzi wa jiwe la msingi wa shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu ya wananchi ambao wametumia kiasi cha shilingi milioni 24, huku kiasi kingine kimeongezewa na serikali na kufikia jumla ya kiasi cha shilingi milioni 45.

Rais Shein amewataka wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanasoma kwani sasa Zanzibar ina shule zaidi ya 200 tofauti na ukilinganisha na hapo awali kabla ya Mapinduzi ambapo kulikuwa na shule sita za serikali ambazo ni wanawake tatu na wanaume tatu. Kiongozi huyo ameongeza kuwa baada ya utawala wa Rais wa kwanza Zanzibar, Abeid Amani Karume ndipo akaamua elimu kutolewa bure kwa wananchi wote.

Ikiwa leo ni siku ya pili ya ziara hiyo katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Wilaya ya Magaribi A, viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Mawaziri, Dkt Shein leo amezindua na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa visima vya maji safi na salama pamoja na kuweka jiwe la msingi katika tawi jipya la CCM lililopo katika eneo la Bumbwisudi.

Wanafunzi wa Skuli ya  msingi Kihinani

Katibu  Mkuu wa Wizara ya Elimu  Khadija Bakari

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki  Pembe Juma

 

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents