Habari

Ziggy Dee wa ‘Eno mic’ adai ukimya wake ulitokana na show nyingi za nje

Msanii kutoka Uganda aliyewahi kuhit hapa Tanzania na single yake ya’ Eno Mic’ aliyofanya na Fatma miaka ya nyuma, amevunja ukimya kwa kutoa single mpya ambayo ameirekodia hapa Taznania.

ZIGGY D

Ziggy Dee amesema ‘Eno Mic’ ilimfungulia milango mingi ya shows, na katika kipindi chote alichokuwa kimya alikuwa akizunguka nje ya Uganda na yote hayo yakiwa ni matunda ya ‘Eno Mic’.

“Nyimbo ya Mic imenipeleka mbali sana kwasababu nimeenda Ulaya sana, Uganda sijakaa kwa sana lakini shows kwa hiyo Mic tuu imenipeleka mbali mabli sana” amefunguka leo Ziggy Dee katika kipindi cha Showtime New Chapter cha Radio Free Africa alipozungumza na mtangazaji wa kipindi hicho Bizzo.

Dee amesema kutokana na kubanwa na ratiba ngumu ya show za nje ndio sbabu alijikuta amekaa kimya kutokana na kukosa muda wa kuandaa kazi mpya.

“Kwa hiyo nilikuwa sipati muda wa studio muda wa kuja huku lakini sasa hivi nimepata nafasi ya kuja huku tena, na nataka nifanye nyimbo nyingi zaidi ya Eno Mic”. Alisema.

Akizungumzia wimbo wake mpya alioutambulisha ‘Livingstone City’, amesema wimbo huo ameufanyia mkoani Tabora alikoenda kufanya show hivi karibuni, na ameelezea sababu kubwa ya kufanya wimbo huo Tabora na sio sehemu nyingine.

“Na kingine nimekuta kuna historical places ambazo hazijulikani kama kwetu, ndio maana nimeamua kufanyia hapa ili na hili jiji litoke kama wasanii wao, kuna wasanii huku nao watasikika tena”.

Msanii huyo ambaye kwao Uganda anamiliki studio yake ya muziki, amewashauri wasanii wa Tanzania kujenga utamaduni wa kujiandalia shows zao wenyewe kama wafanyavyo wasanii wa Uganda, ili kujitengenezea pesa zaidi kuliko kutegemea mapromota.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents