Burudani

Zomba Prison Project: Bendi ya wafungwa wa Malawi iliyotajwa kuwania tuzo za Grammy

Kwenye sauti utamkuta, Elias Chimenya aliyefungwa kwa mauaji, gitaa la besi, jambazi, Stefano Nyerenda huku askari, Thomas Binamo akiwa mmoja wa waandishi wa nyimbo za kundi hili.

malawi-prison-band-vies-for-grammy-glory-1452622301-2005

Bendi ya Zomba Prison Project ya Malawi itawania tuzo za Grammy zitakazotolewa mwezi ujao nchini Marekani. Albamu yao yenye nyimbo 20, ‘I Have No Everything Here’ ilitajwa kuwania kipengele cha Best World Music Album kwenye tuzo hizo.

Kundi hilo lilianzishwa mwaka 2013 kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Zomba baada ya mtayarishaji wa muziki wa Marekani, Ian Brennan alipotumia wiki mbili kutengeneza albamu hiyo na wafungwa 60.

Elias Chimenya, 46, anayetumikia kifungo cha maisha kwa kumuua mtu kwenye ugomvi miaka ya 1980, aliandika wimbo uitwao ‘Jealous Neighbour.’

Amesema muziki umemfanya awe mtulivu na kuzoea maisha ya jela. “Ninaamini sitafia jela, badala yake nitaachiwa ili nikaendelea na muziki nje,” aliliambia shirika la AFP.

Wamesema kutajwa kwenye tuzo za Grammy ni kitu ambacho hawakukitegemea.

“Tumeshangazwa kwasababu hatukutegemea wafungwa kutajwa,” alisema Nyerenda, 34 anayetarajia kutoka jela mwakani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kufanya tukio la ujambazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents