Muziki

Zuchu aongoza wasanii wa kike Afrika Mashariki nyimbo zake kutazamwa zaidi YouTube

Mwimbaji kutokea WCB Wasafi, Zuchu amefanikiwa kuingiza nyimbo nne katika orodha ya video 10 za wasanii wa kike Afrika Mashariki zilizotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa muda wote.

Wasanii wengine kutoka Tanzania waliongia katika orodha hiyo ni Maua Sama, Queen Darleen na Nandy, huku Kenya ikitoa wasanii wawili ambao ni Tanasha na Mwimbaji wa Injili, Mercy Masika.

Wimbo wa Zuchu ‘Sukari’ ndio umeongoza ukiwa na views Milioni 44, Cheche umekamata nafasi ya nne, views milioni 22, Litawachoma nafasi ya sita, views milioni 17 na Wana nafasi ya 10, milioni 13.

Tanasha kutokea Kenya, wimbo wake ‘Gere’ alioshirikiana na Diamond Platnumz umekamata nafasi ya pili ukiwa na views milioni 26. Nafasi ya tatu kaichukua Maua Sama kupitia wimbo ‘Iokote’ aliomshirikisha Hanstone ambao una watamazaji views Milioni 22.

Queen Darleen ambaye naye anatokea WCB kashika nafasi ya tano kupitia wimbo ‘Kijuso’ alioshirikisha Rayvanny, huu una views milioni 20.5. Namba saba kaichukua Nandy na wimbo wake ‘Ninogeshe’ wenye views milioni 15, pia kaichukua na namba tisa kupitia wimbo ‘Kivuruge’ wenye views milioni 13. Kisha Mkenya, Mercy Masika na wimbo ‘Mwema’ uliojipatia views Milioni 14 akaichukua nafasi ya nane.

Katika orodha hiyo Tanzania imetoa wasanii wanne waliochangia nyimbo nane, huku Kenya ikitoa wasanii wawili waliochangia nyimbo mbili pekee. Nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini ambazo nazo zinaunda Jumuiya ya Afrika Mashariki, hazijafanikiwa kuingiza msanii yeyote.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents