Burudani

Adam Juma ashauri wasanii kufanya show ya bure kuhamasisha bunge la katiba kuingiza sanaa katika katiba mpya

Wiki iliyopia baadhi ya mastaa wa Hip Hop wa Tanzania waliungana katika studio ya Bongo Records kufanya wimbo wa pamoja uitwao ‘Haki’, kwaajili ya kampeni ya kulihamasisha bunge maalum la katiba kuiweka sanaa na haki za kazi za kiubunifu yaani (Intellectual Property) katika katiba mpya.

HAKI-Cover-2

Mtayarishaji wa video wa Next Level Adam Juma, ametoa ushauri kwa wasanii na wadau wote wa sanaa kufikiria swala la kufanya show ya bure na mandamano ya amani kama njia ya kupaza sauti iwafikie wabunge wa bunge maalum la katiba kuhusiana na matakwa ya wasanii.

Adam Juma

“Hivi hatuwezi kweli kufanya show moja bure na maandamano ya amani ili sauti yetu isikike bungeni sanaa itambulike kwenye katiba yetu! Radio zote, tv zote, wasanii wote film/music, producers wote, waandishi wote n.k ni wazo tu”. Aliandika Adam Juma Instagram.

Hata hivyo hakuna msanii hata mmoja aliyechangia chochote katika mawazo yake hayo kwenye post yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents